
NAIROBI, KENYA, Julai 25, 2025 — Robert Alai amemtaka Katibu Mkuu wa ODM, Edwin Sifuna, kujiuzulu kutoka chamani iwapo hawezi kuelewana na msimamo wa kinara Raila Odinga kuhusu kushirikiana na Rais William Ruto.
Katika kile kilichoonekana kama mashambulizi makali ya kisiasa, Diwani wa Wadi ya Kileleshwa, Robert Alai, amemshambulia vikali Katibu Mkuu wa ODM Edwin Sifuna, akimtuhumu kwa kujaribu kumhujumu Raila Odinga kupitia mikakati ya chini kwa chini.
Alai: Sifuna Amekuwa Kizuizi, Sio Mchango
Alai alidai kuwa Sifuna alitumia Seneta Osotsi kuandaa kongamano la wajumbe kule Kakamega kwa nia ya kumbana kisiasa Raila Odinga.
"Seneta Edwin Sifuna alitumia Seneta Osotsi kuandaa kongamano la wajumbe Kakamega ili kumlaghai Raila, alisema Alai.
Alai aliendelea kumkosoa Sifuna kwa madai ya kutumia wanasiasa wasio na ushawishi kujijenga kisiasa ndani ya chama.
"Sifuna kisha akatumia kundi lisilo na elimu kama Raphael Wanjala kudai kwamba ni Waluo pekee wanaomchukia."
"Sifuna Yuko Peke Yake" – Alai Asema
Alai alidai kuwa viongozi wakongwe ndani ya ODM wamejitokeza kuonesha kuwa hawamuungi mkono Sifuna, akiwataja Gavana Paul Otuoma na Mbunge John Waluke Barasa kama mifano.
"Mbali na wale Sangwenya wachache aliowalipa kumpigia makofi, Sifuna yuko peke yake katika mawazo yake. Wakongwe kama Gavana Otuoma na Barasa wameshaonesha hivyo."
Kwa mujibu wa Alai, Raila Odinga mwenyewe pia ametoa msimamo wazi kuhusu kutokubaliana na misimamo mikali ya Sifuna.
"Baba Raila alihitimisha na kuonesha kwamba havutiwi na mawazo ya kuextremist ya Sifuna."
“Sifuna, Ondoka ODM Kama Hukutosheka”
Katika ujumbe wake wa mwisho, Alai alimtaka Sifuna kuondoka ODM ikiwa hawezi kuelewana na mwelekeo mpya wa chama.
"Ujumbe umefika nyumbani. Sifuna, kama hutosheki ODM, ondoka. Unaweza ondoka na Seneta Sosa kama Osotsi pia. Mbali na malumbano, hawaleti faida yoyote kwa ODM."