
NAIROBI, KENYA, Agosti 1, 2025 — Maafisa kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) wamemkamata afisa wa zamani wa polisi Hiram Kimathi nyumbani kwake eneo la Kambakia, Makutano, Kaunti ya Meru, kwa tuhuma zinazohusiana na kuundwa kwa kundi la kupinga ukatili wa polisi linalojulikana kama FBI (Fighting Brutality and Impunity).
Kukamatwa kwa Kimathi kunakuja siku chache tu baada ya wenzake Jackson Kuria almaarufu Cop Shakur na Patrick Osoi kutiwa nguvuni, wote wakihusishwa na harakati za kupinga amri haramu na ukatili wa maafisa wa usalama.

Kimathi Akamatwa Bila Kufahamishwa Sababu
Masaibu ya Kimathi yalianza majira ya saa saba mchana wakati maafisa wa DCI walipovamia makazi yake na kumsihi kutoka nje.
Alipotekeleza agizo hilo, alifungwa pingu na kupandishwa kwenye gari la Subaru kisha kupelekwa kusikojulikana.
Kiruai alieleza kuwa vitendo vya Kimathi na wenzake katika kundi la FBI vinaangukia ndani ya uhuru wa kujieleza unaolindwa na Katiba ya Kenya.
Kundi la FBI na Tuhuma za Kuvuruga Usalama
Kwa mujibu wa hati ya ombi iliyowasilishwa na DCI mahakamani, Patrick Osoi—ambaye pia alikamatwa wiki hii na kufikishwa katika Mahakama ya Kahawa—alidaiwa kuunda kundi la FBI pamoja na Cop Shakur na Kimathi.
FBI, kwa mujibu wa DCI, inalenga kushawishi maafisa wa zamani na waliopo kupinga “amri zisizo halali” zinazotolewa na serikali.
Katika machapisho yake ya mitandaoni, Osoi alitangaza nia ya kuwania urais mwaka wa 2027 kupitia mrengo wa FBI.
Inasemekana kuwa mbali na kuwa mwanajeshi wa zamani wa KDF, Osoi pia ni mkongwe wa Jeshi la Marekani (US Army) na amejitambulisha kama afisa wa zamani wa Huduma ya Ujasusi ya Kitaifa (NIS).
Maafisa Waliotengwa Wajitokeza Kutetea Raia dhidi ya Ukatili wa Polisi
Cop Shakur Apigwa Mtego Mahakamani
Jackson Kuria almaarufu Cop Shakur, alikamatwa siku hiyo hiyo ya Jumatano alipofika Mahakama ya Kahawa kuunga mkono Osoi wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake.
Osoi anakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwa ni pamoja na:
Hiram Kimathi, afisa wa zamani wa polisi, amekamatwa na maafisa wa DCI kwa tuhuma za kuhusika na kundi la FBI linalopinga ukatili wa polisi. Kukamatwa kwake kunafuatia msururu wa matukio yanayowahusisha wenzake Cop Shakur na Patrick Osoi.