Aliyekuea muigizaji wa kipindi cha Maria kwenye runinga ya Citizen, Wanjiku Stephens ambaye wengi walimfahamu kwa jina la uigizaji la Vanessa Hausa amekuja na jipya kabisa kutoka jikoni.
Vanessa anadhihirisha wasiwasi wake kwa mashabiki wake kwenye mtandao wa Instagram, ambapo alipakia video akieleza kufadhaika kwani mwaka unaisha na bado hajapata mama mkwe.
Kupitia video hiyo aliyoipakia kwenye instastories zake, Vanessa alisema kwamab anahitaji mwanaume wa kumuoa na kuwataka wanaume wote huku nje wenye nia njema ya kutuma posa kwake kufanya hivo kabla mwaka huu haujaisha kwani ni miezi michache tu imebakia kabla ya kuufunga kabisa.
“Nahitaji mwanaume. Mwaka mwingine mzuri unaisha na bado sijapata mama mkwe, si mtu mmoja tu ajitolee abadilishe hii hali,” Vanessa Hausa alisema kweney video hiyo.
Hausa alikuwa anaigiza na wenzake wengi katika kipindi hicho cha Maria ambacho kilikamilika miaka miwili iliyopita.
Mashabiki wake walifurika kwenye video hiyo na kuachia maoni yao huku wengine wakimtania kwamba aliwakataa na baadhi wakimwambia watamfanyia maombi kwa ajili ya kutimiziwa hilo.
“Nitakufanyia crusade.. 😂😂 Tuombe kama taifa! Siku ya maombi ya kaunti ya Nairobi kwa wake watarajiwa,” mtangazaji Mike Mondo alimtania.
“Si ulinikataa eti mimi ni mtanashati zaidi,” mchekeshaji Sleemtee alimwambia.
Wengine walimtaka kujibu meseji zao katika DM huku wengine pia wakimwambia kwamba huenda anawatupia mchanga machoni kwani kwa urembo na ulimbwende aliokuwa nao ni vigumu sana kuwa hana mwanaume mpaka sasa.