Msanii Nandy na Baba Levo wametupiana maneno makali kuhusu msanii wake mpya kwa jina Yummi.
Zogo lilianza wakati Nandy alipakia kionjo cha msanii wake mpya Yummi akiwa kwenye lokesheni akifanya wimbo na kumsifia kuwa wimbo wake ulikuwa mkali zaidi ya mbwa wa kizungu.
“HANIPENDI MOVIE π…….. HAKA KA wimbo bwana ni nomaaa sana,” Nandy aliandika kwenye kionjo cha video hiyo ya msanii wake huku akiwahimiza watu waendelee kuutazama wimbo huo kwenye mitandao yote ya kijamii pamoja na majukwaa ya kupakuwa miziki.
Hapo ndipo mchokozi Baba Levo aliandika tamko la kukejeli akisema kuwa msanii wa Nandy alikuwa amepoa kuliko ugali wa juzi, akiweka na emoji za kucheka kwa kejeli.
“Msanii Amepoooza kama ugali Wa Jana ππππππππππ” Baba Levo alichokoza.
Tamko hili halikukaa vizuri na Nandy ambaye alimrukia kichwani Baba Levo kama nyoka wa kufutu, huku akimdhalilisha kuhusu pua lake kuwa ni kubwa.
Ikumbukwe hii si mara ya kwanza kwa chawa huyo wa Diamond kutukanwa kuwa pua lake ni kubwa, jambo ambalo hata yeye mwenyewe kipindi kimoja alizungumzia na kukiri kuwa amekuwa akikebehiwa na umbile la pua lake huku akisema kuwa amekuwa akitathmini siku moja kuendea huduma za upasuaji ili kupunguza ukubwa wa pua lake – upasuaji kama ule ambao mkongwe wa muziki kutoka Marekani Michael Jackson aliwahi fanyiwa.
Nandy alisema mashabiki wake wanampenda hivo hivo huku akimtaka Baba Levo kukoma kumkandia msanii mpya na badala yake kumuunga mkono ili alete ushindani kwa muziki.
Nandy alimzindua msanii huyo wake mpya kwenye lebo yake ya African Princes, lebo ambayo alisema itakuwa ni ya kusaini watoto wa kike pekee ili kuwainua pia kufikia kiwango cha wasanii wa kiume.