Mwanamke wa miaka 24 atiwa mbaroni katika kijiji cha South Gate, eneo bunge la Butula , kaunti ya Busia baada ya kumdunga jamaa mmoja hadi kufa na makasi mara saba.
Mhusika Joyce Atieno Odhiambo alihusikia katika kitendo hicho cha kinyama baada ya kumuua mpenziwe wa miaka 29 kwa jina la Lucas Onyango huku akitumia makasi.Chanzo cha Joyce kumdunga mmewe bado akijajulikana lakini inakisiwa huenda ikwa ni mzozo wa kifamilia .
Kulingana na ripoti iliyotolewa na polisi ni kwamba Onyango alipoteza maisha yake baada ya kuuguza majeraha hayo akiwa anaendelea kupata matibabu.Polisi wakiongozwa na OCS wa Bumala walithibitisha habari hiyo na kusema mwendazakev aliuguza majeraha makali ya kudungwa na makasi na mkewe.
Baada ya mfarakano huo na mkewe Lucas alikimbizwa hosipitali ya Sega Mission kupata matibabu lakini hali ikashindikana na kupelekea kupoteza maisha yake.
Baada ya polisi kufika katika eneo la tukio waliweza kupata idhibati ikiwemo makasi iliyotumika kumtoa Lucas uhai, nguo ambazo zilikuwa zimejaa damu za mwendazake pamoja na za mhusika.
Mhusika alitiwa mbaroni na anaendelea kuzuiliwa katika kituo cha pilisi cyha Butula huku mwili wa mwendazake ukitarajiwa kufanyiwa upasuaji ili kubaini chanzo kamili.