logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Washukiwa wa ulanguzi wa binadamu wakamatwa Kitengela

Watu hamsini na wanane wameokolewa na polisi wakiwa tayari kusafirishwa kuelekea taifa la Afrika Kusini

image
na Evans Omoto

Yanayojiri05 February 2025 - 16:04

Muhtasari


  • Kwenye maeneo ya tukio hilo kulipatikana  pikipiki aina yenye nambari ya usajili KMGK 123T ambayo ilibebwa na maafisa wa polisi na kupelekwa katika kituo cha Kitengela ili kusaidia polisi kwa uchunguzi wa undani.

Watu hamsini na wanane wameokolewa na polisi wakiwa tayari kusafirishwa kuelekea taifa la Afrika Kusini.

Katika oparesheni iliyoendeshwa kwa ushirikiano kati ya maafisa ya kitengo maalum cha kukabiliana na uhalifu pamoja na maafisa wa polisi kutoka kituo cha Kitengela inasemekana kuwa watu hawa walikuwa katika harakati za kusafirishwa kuelekea taifa la Afrika Kusini.

Kutokanna na taarifa iliyopashwa maafisa wa polisi kutoka kwa mwananchi ambaye alishuku kuwepo kwa watu fulani katika nyumba maalum iliyoko karibu na nyumba ya Huduma(House of Delivarance) iliyoko katika maeneo ya Kitengela kufuatia operesheni hiyo ya kuwaokoa matekwa pamoja na kukamata wahusika, washukiwa wawili walikamatwa kusaidia polisi kwa uchunguzi.

Mshukiwa Daniel Nduati Kingoo na Peter Maina Kimemia walikamatwa ili kuwasaidia polisi kutegua kitandawili hicho cha ni kwa nini watu zaidi ya 58 wangepatikana katika jengo moja mahali pamoja kwa wakati mmoja tena wakiwa wengi kupita kiasi ,hayo majibu wawili hao watasaidia polisi kujibu na ikiwa watapatikana na hatia kwa namna moja au nyingine sheria itachukua mkondo wake.

Kulingana maelezo ya kuaminika ambayo yalichapishwa katika ukurasa wa DCI yanasema kuwa kati ya matekwa hao 58 ishirini na wanane wamepelekwa katika kituo cha Polisi cha Kitengela huku thelathini wakihamishiwa kituo cha polisi cha Isinya na washukiwa wakuu wakipelekwa katika kituo cha polisi cha Muthaiga ili kusaidia polisi kupambanua suala hili.

Kwenye maeneo ya tukio hilo kulipatikana pikipiki aina ya Honda yenye nambari ya usajili KMGK 123T ambayo ilibebwa na maafisa wa polisi na kupelekwa katika kituo cha Kitengela ili kusaidia polisi kwa uchunguzi wa undani.

Kulingana na mujibu wa sheria za Kenya kuhusu ulanguzi wa binadamu sheria inaelezea vyema katika kipengee cha mwaka 2010 ambayo inaharamisha ulanguzi wa binadamu na kuvutia adhabu kali kwa yeyote yule atakayehusika katika kitendo hicho haramu.

Iwapo utapatikana ulihusika au kuendeleza vitendo vya ulanguzi wa binadamu utakabiliwa na mkondo wa sheria ambapo utafungwa jela miaka thelathini au utozwe faini ya shilingi milioni thelathini au vyote viwili sheria inafafanua.

Makala Zinazohusiana

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved