

Mwenyekiti
wa Kamati PAC Mbunge wa Butere Tindi
Mwale, baada ya uchaguzi wa kamati Machi 12, 2025
Mbunge wa Butere Tindi Mwale amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Kitaifa ya Uhasibu wa Umma (PAC).
Mwale alimbwaga mpinzani wake wa karibu, Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo kwa kura tisa dhidi ya sita za Otiende.
Mwale amekuwa akihudumu kama kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo, tangu mwenyekiti aliyekuwepo John Mbadi alipoteuliwa kuwa waziri wa fedha.
Mwakilishi wa Wanawake wa Garissa Amina Siyad alimshinda Mbunge wa Funyula Dkt Wilberforce Oundo kutwaa nafasi ya naibu mwenyekiti.
Wakati huo huo Mbunge wa Pokot Kusini David Pkosing amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji wa Umma kuhusu Masuala ya Biashara na Nishati bila kupingwa.
Alihifadhi kiti hicho katika huku Mbunge wa Turkana Kusini John Ariko akichaghuliwa naibu mwenyekiti.
Pkosing aliwashukuru wanachama wa kamati hiyo na viongozi wa serikali mahuluti (Broad Based government) - Rais William Ruto na Raila Odinga—kwa kumkabidhi jukumu hilo.
"Ninaamini huu ni mwanzo wa uwiano na utangamano kati ya Waturkana na Pokot," Mbunge wa Laikipia Magharibi Sarah Korere alisema.
Pkosing alisema kuteuliwa kwake na Ariko ni ushahidi kwamba jamii hizo mbili si maadui. Akisema kamati hiyo itayapa kipaumbele maswala muhimu yanayohusu wananchi.