logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kenya Power yatangaza maeneo yatakayokumbwa na kukatika kwa umeme leo Alhamisi

Kenya Power limetangaza kuwa baadhi ya maeneo nchini yatakumbwa na kukatika kwa umeme Alhamisi, Machi 13, 2025.

image
na Samuel Mainajournalist

Yanayojiri13 March 2025 - 07:03

Muhtasari


  • Kwa jumla, maeneo katika kaunti 11 yatakosa umeme kwa muda tofauti kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. 
  •  Kaunti zitakazoathirika ni Nairobi, Machakos, Kiambu, Murang’a, Mombasa, Marsabit, Tharaka Nithi, Nyeri, Meru, Kakamega, na Vihiga.

KPLC

Shirika la Kenya Power limetangaza kuwa baadhi ya maeneo nchini yatakumbwa na kukatika kwa umeme Alhamisi, Machi 13, 2025, ili kuruhusu matengenezo ya mfumo wa usambazaji.

Kwa jumla, maeneo katika kaunti 11 yatakosa umeme kwa muda tofauti kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti zitakazoathirika ni Nairobi, Machakos, Kiambu, Murang’a, Mombasa, Marsabit, Tharaka Nithi, Nyeri, Meru, Kakamega, na Vihiga.

Nairobi

Katika jiji la Nairobi, umeme utakatika kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Maeneo yatakayoathirika ni Barabara ya Murang’a, Hospitali ya Gurunanak, Kituo cha Polisi Pangani, Barabara ya Juja, Hospitali ya Radiant, Barabara ya North View, Strawberry, na maeneo jirani.

Vilevile, sehemu ya Barabara ya Mbagathi, Akila Estates, Miller Estate, Civil Servant Estate, Hamayun, Akiba Estate, Muslim Academy, Kinder World, Airport View Estate, White Star Academy, Bible Society, sehemu ya Barabara ya Lang’ata, AP Camp Mbagathi Road, Kwetu Hostels, na Chuo cha Strathmore zitakosa umeme kwa muda huo.

Machakos

Katika Kaunti ya Machakos, umeme utakatika kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Maeneo yaliyoorodheshwa ni Makutano Mwala, Mwala, Kivandini, Mbiuni, Ghetoo, Wamunyu, Yathui, Ikalaasa, Tulila, Miondoni, Syokisinga, Katangi, Ikombe, Kenyaata, Chuo Kikuu cha Seku, Kyua, na maeneo jirani.

Kakamega

Kaunti ya Kakamega pia itaathirika na mgao wa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Maeneo yatakayokumbwa na hali hiyo ni Hospitali ya Igukhu, Makhokho, Khaega, na maeneo jirani.

Vihiga

Maeneo ya Kaunti ya Vihiga yatakayokosa umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni ni Kituo cha Mafuta cha Shell Luanda, Kituo cha Polisi cha Maseno, Sunrise, Maseno Ekwanda, Maseno Sunga, Holo, Magwar, Emaloba, Khiliba, Maseno Depo, Bishop Olang, na maeneo jirani.

Nyeri

Katika Kaunti ya Nyeri, umeme utakatika kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Maeneo yaliyoathirika ni Muruguru Kwa Kigera, Kiwanda cha Vet Pro, Shule ya Msingi na Kanisa Katoliki la Kiamuiru, Hoteli ya Mugwathi, Satima Millers, Kituo cha Mafuta cha Royal, Soko la Githiru, Kiwanda cha Githiru, na maeneo jirani.

Meru

Maeneo kadhaa katika Kaunti ya Meru yatakosa umeme kati ya saa mbili na nusu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Miongoni mwa maeneo haya ni Mucuune, Maliolo, Shule ya Msingi ya St. Stephen, Shule ya Msingi ya St. Benedict, Shule ya Msingi na Sekondari ya Kiguchwa, Kiguchwa Safaricom, Shule ya Msingi ya KK Mwethe, Shule ya Sekondari ya Kaliene, Ametho Boarding, St. Lucy Kirigwa, Ankamia Mixed Day Secondary, Ankamia Primary, Kituo cha Biashara cha Ngutu, Shule ya Sekondari ya Miurine, Kijiji cha Karurune, Masoko ya Gachuuru na Githu, Shule ya Sekondari ya Githu Mixed, Kiarau, Shule ya Sekondari ya Irindiro, Kieni TBC, Amungaa, Murichia C/Fact, na maeneo jirani.

Sehemu nyingine zitakazokumbwa na hali hiyo ni Safaricom Kiirua, Hoteli ya Sera Park, Mboroga, Meru Central Kiirua, Soko la Kibithe, Mborione, Soko la Mutungi, Shule ya Sekondari ya Gakando, Kijiji cha Gakando, Machaka Slums, Soko la Ntugi, Shule ya Sekondari ya Ntugi, Shule ya Msingi ya Karanene, na Soko la Kirima Kia Itunga.

Maeneo mengine ya Meru yatakayokumbwa na mgao wa umeme kuanzia saa mbili asubuhi ni Kariene, Rwankare, Shule ya Msingi ya Gitauga, Shule ya Msingi ya Tabata, Chuo cha Vijana cha Kiamakoro, Ntimene, Shule ya Msingi ya Rwangua, Soko la Kaogo, Shule ya Msingi ya Mutharene, Kiwanda cha Muturia, Shule ya Msingi ya Gatenderene, Ntharagwene, na Shule ya Msingi ya Karia ka Ngogo.

Tharaka Nithi

Kaunti ya Tharaka Nithi itakosa umeme kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Maeneo yatakayokosa umeme ni Karamani, Shule ya Sekondari ya Kanyuru, Soko la Cheera, Shule ya Msingi ya Ikawa, Eneo la Kwa Mate Stage, Kijiji cha Ithima, Kiwanda cha Nthima, Shule ya Bweni ya Salama, na maeneo jirani.

Marsabit

Sehemu za Kaunti ya Marsabit zitakumbwa na kukatika kwa umeme kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa tisa alasiri. Maeneo yaliyoathirika ni Mji wa Moyale, Hospitali ya Moyale, Zahanati ya Somary, Gereza la Moyale, Shule ya Wavulana ya Moyale, Zahanati ya Odda, Msikiti wa Kinisa, na maeneo jirani.

Murang’a

Katika Kaunti ya Murang’a, umeme utakatika kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Maeneo yaliyoathirika ni Githingiri Estate, Golf View Estate, Thika Greens, Jowaki Farm, Thika Green Golf Club, KARLO, Mugumo Farm, Brush Industries, Kandara Business Park, Vijiji vya Rwathe, Mukuria, na Ruona, Masoko ya Gacharage, Muruka, na Ngararia, pamoja na maeneo jirani.

Kiambu

Kaunti ya Kiambu pia itakosa umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Maeneo yaliyoathirika ni Shule ya Upili ya Kahuho, Shule ya Wavulana ya Kirangari, Nyathuna, sehemu ya Gitaru, Chura, Soko la Ruku, Gwa Thiongo, na sehemu ya Lower Kabete Junction.

Mombasa

Katika Kaunti ya Mombasa, umeme utakatika kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Maeneo yaliyoathirika ni East African Storage, Gulf Stream, Vivo Energy, na maeneo jirani.

Shirika la Kenya Power limewataka wateja walioko katika maeneo haya kuchukua tahadhari na kupanga shughuli zao ipasavyo wakati wa muda wa kukatika kwa umeme.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved