logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC Yatangaza Maeneo Ambayo Yatakosa Umeme Leo, Jumanne

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Februari 25.

image
na Samuel Mainajournalist

Yanayojiri25 February 2025 - 08:18

Muhtasari


  • Kampuni ya KPLC imesema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
  • Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Narok, Bungoma, Nyeri, Embu, Kiambu, na Kilifi.

kplc

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Februari 25.

Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Narok, Bungoma, Nyeri, Embu, Kiambu, na Kilifi.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Jogoo Road, Tassia, Kilimani, Woodley, Jamhuri, na Kibera zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo ya Ololunga na Ngoringori katika kaunti ya Narok zitaathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi alasiri.

Soko la Bukembe katika kaunti ya Bungoma pia litaathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na mbili jioni.

Katika kaunti ya Nyeri, maeneo ya Gatondo Market, Kigogoini, na Kiriti yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo Ndumboini, Uthiru, Bluepost, na Bendor zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Eneo la Pwani University pia litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.


Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved