
Jopokazi lililoteuliwa ili kuwapiga msasa wanachama na kumteua mwenyekiti wa IEBC limemtema Oswogo.
Katika uteuzi ambao majina ya wanachama yaliweza kurodheshwa
katika harakati za kumtafuta mwenyekiti mpya wa IEBC.
Baadhi ya wagombeaji walionyesha ari ya kusaka nafasi hiyo
ambao majina yao yaliweza kurodheshwa ili kujiandaa kwa kuweza kupigwa msasa na kamati ya jopo hilo ni Jaji wa zamani wa mahakama ya Afrika Mashariki
Charles Nyachae na aliyekuwa msajili mkuu wa zamani wa mahakama Anne Amadi.
Katika notisi iliyotolea siku ya Ijumaa Machi, 2025 Bwana
Nelson Makanda aliongoza jopo la uteuzi akisema kuwa mahojiano ya moja kwa moja
yatafanyika kwa wagombeaji kumi na mmoja (11) kati ya Machi 24,2025 na Jumatano
Machi 26,2025.
Wawaniaji wengine waliokimezea mate kiti hicho ni aliyekuwa
naibu msajili wa mahakama Bwana Kakai Kissinger na Mwenyekiti wa Kenya Power
Joe Mdivo aliyehudumu katika kampeni za rais William Ruto 2022 na kwenye kamati
ya chama cha UDA.
Aliyekuwa afisa mkuu mtendaji wa IEBC bwana James Oswago
alitemwa baada ya kutajwa katikA orodha
ya watu 37 walioonyesha ari ya kutaka kutwaa nafasi hiyo ya uenyekiti wa IEBC
Bila kufanikiwa.
Mahojiano ambayo yatafanyika katika ukumbi wa Ballroom afisi za bima ya uwekezaji katika maeneo ya South C. Ratiba ya utaratibu wa watakaohojiwa imetolewa .
Atakayekuwa wa kwanza kuhojiwa mnamo Machi 24,2025 ni
Abdulqadir Lorot kwanzia saa 8:30 asubuhi, Hatimaye Anne Amadi saa 11:00, Charles Nyachae saa 2:00
adhuhuri na Edward Katana Ngeywa saa
4:30 alasiri.
Siku ya Jumanne Machi 25,2025 Erastus Ethekon
atahojiwa sa 8:30 asubuhi akifutwa na Kakai Kassinger saa 11:00,Jacob Muvengei
saa 2:00 adhuhuri na baadaye Joy Mdivo akamilishe siku saa kumi unusu jioni 4:30.
Siku ya Jumatano Machi 26,2025 Lilian Wanjiku atajitosa mbele ya jopo la usaili saa 8:30 asubuhi akifuatwa na Robert
Akumu Asembo saa 11:00 na hatimaye Sauli
Simiyu Wasilwa akamilishe saa 2:00 alasiri.
Hata hivyo jopo la
uteuzi pia liliweza kuwarodhesha wawaniaji
110 waliotuma maombi ya kujaza nafasi za makamishina .
Mahojiano kwa ajili ya makamishina yataanza siku ya Alhamisi
Machi 27,2025 hadi Alhamisi Aprili 24,2025.
Wawaniaji wote wameelezwa kuwa mahojiano yatafanyika kwa
uwari mbele ya umma hivyo waliombwa wawe na stakabadhi muhimu na waweze kuwa na
barua kutoka kwa asasi kama vile tume ya madilim na kupambana na ufisdi EACC
,idara ya upelelzi wa makosa ya jinai DCI
na ofisi ya ukusanyaji wa ushuru KRA.
Hatimaye jopo litateua majina mawili na kumpokeza rais ambaye atachagua mmoja wao
kama mwenyekiti wa tume ya IEBC, vilevile jopo litapendekeza majina tisa ya
makamishina wa IEBC ambapo rais atateua makamishina sita.