
Mwanafunzi wa chuo kikuu aliyehusishwa na mauaji ya mwanafunzi mwenzake katika Chuo Kikuu cha Multimedia (MMU) alijisalimisha kwa mamlaka siku chache baada ya kukimbia.
Polisi walisema mshukiwa, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Uhandisi wa Umeme, pia ni mwanafunzi katika chuo hicho cha MMU.
Kamanda wa Polisi wa Nairobi George Sedah alisema mshukiwa alijisalimisha katika kituo cha polisi cha Sultan Hamud huko Makueni Alhamisi usiku baada ya kuhusishwa na mauaji ya Sylvia Kemunto, ambaye alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Mawasiliano na Sayansi ya Kompyuta.
Mshukiwa huyo alikuwa mafichoni tangu Jumatatu iliyopita wakati anaaminika kuua na kuutupa mwili wa Kemunto kwenye tanki la maji ndani ya chuo hicho.
Sedah alisema timu kutoka Nairobi ilikuwa imesafiri hadi kituo cha polisi cha Sultan Hamud kumchukua mshukiwa.
"Ni bahati mbaya kwamba msichana aliuawa. Tunaamini yeye ni mshukiwa mkuu wa mauaji hayo, na timu imeenda kumchukua," alisema.
Inaaminika alitorokea nyumbani kwao mashambani baada ya mauaji hayo. Alisema wanataka kuelewa ikiwa alikuwa ametenda peke yake na motisha yake ilikuwa nini.
Utafutaji wa Kemunto ulianza Jumapili, Machi 30, wakati mama yake, Triza Kwamboka, anayeishi Kawangware, Nairobi, aliposhindwa kumfikia.
Alisema alikuwa amemtumia pesa za utunzaji kupitia simu ya mzee wa kanisa, lakini simu zake hazikujibiwa alipojaribu kuthibitisha ikiwa binti yake alikuwa amepokea pesa hizo. Akiwa na wasiwasi, mama ya Kemunto alisafiri kwenda chuo kikuu, na kugundua kuwa binti yake hayupo.
Uongozi wa chuo hicho ulithibitisha kutokuwepo kwake, na kumfanya mama huyo kuwasilisha ripoti katika Kituo cha Polisi cha Langata.
Mama huyo aliwaambia polisi Kemunto alikuwa amelalamika juu ya mwanafunzi mwenzake ambaye alikuwa amemtishia kwamba anataka wawe naye kwenye mahusiano ila aliishi kukataa.
Alisema hampendi, na nilimwambia asimame kidete," alisema Kwamboka.
Uchunguzi wa polisi unaonyesha mwanafunzi huyo anaweza kuwa aliuawa chumbani kwake na mwili wake baadaye uliburuzwa hadi juu ya paa la hosteli kwenye matangi ya maji na kutupwa humo
Wauaji kisha walifunga tanki na waya na kuweka jiwe hapo, dhahiri kuzuia kugunduliwa chochote.
Siku ambayo Kemunto alipotea, mwenzake alisema alienda kanisani na kumwacha peke yake chumbani. Siku hiyo, mpenzi huyo alimtembelea chumbani kwake mwendo wa mchana.
Mashahidi waliwaambia polisi baadaye walimwona mtu huyo akivuta begi la mwanafunzi aliyekufa kutoka chumbani humo hadi chumbani kwake katika eneo tofauti.
Inashukiwa kuwa begi hilo lilikuwa na mwili wa mwanadada huyo. Baadaye usiku huo, mwenzake waliyekuwa wakiishi na yeye aliripoti kugundua begi hilo chumbani mwao, lakini lilikosekana asubuhi iliyofuata.
Shahidi huyo alisema alimuona mshukiwa akiwa amelalia kwenye begi hio lakini hakuelewa motisha ilikuwa nini.
"Asubuhi iliyofuata, niliamka karibu saa mbili na nikagundua kuwa Roommate wangu hayuko na begi hilo pia halipo.," shahidi alisema.
Kaimu Makamu wa chuo hicho Prof. Geoffrey Kihara alisema polisi wanachunguza mauaji hayo.