
Kampuni ya kusambaza umeme nchini Kenya Power (KPLC) imetangaza kukatika kwa umeme katika maeneo mbalimbali ya kaunti tisa siku ya Jumanne, Aprili 8, ili kuruhusu matengenezo ya mifumo ya usambazaji wa umeme.
Kaunti zitakazoathirika ni Nairobi, Nyandarua, Uasin Gishu, Tharaka Nithi, Nyeri, Laikipia, Siaya, Kisii na Kirinyaga.
Umeme utakatika kwa nyakati tofauti kati ya saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni, kutegemea eneo.
Nairobi
Sehemu za Nairobi zitakumbwa na kukatika kwa umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Maeneo yatakayoathirika ni:
- Sehemu ya Barabara ya Karen
- Mbagathi Ridge
- Cemastea
- Oloolua Nature Trail Primate Research
- Gitamuri na maeneo ya karibu
Nyandarua
Katika kaunti ya Nyandarua, maeneo yote ya Kinamba yatakosa umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Maeneo hayo ni:
- Muthengera
- Kwanjiku
- Mochongoi
- Kabel
- Tandare
- Kamwenje
- Oljabet
- Gatundia
- Karaba
- Mutanga
- Sipli
- Olmora
Uasin Gishu
Maeneo ya Uasin Gishu yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri. Maeneo ni:
- Kipkenyo
- Tuiyo
- Leemok
- Simat
- Kaptinga
- St. Teresa na wateja wa karibu
Siaya
Maeneo ya Siaya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Maeneo husika ni:
- Nyumbani Shop
- Shule ya Msingi ya Anduro
- Soko la Randago
- Shule ya Upili ya Matera
- Soko la Tingwangi
- Shule ya Upili ya Nyajuok
- Booster ya Safaricom ya Nyanginja
- Vyuo vya Ufundi vya Nyala
- Soko la PapGori
- Shule ya Upili ya Ojwando na maeneo ya karibu
Kisii
Katika kaunti ya Kisii, taasisi na masoko kadhaa yatakosa umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Maeneo hayo ni:
- Shule ya Upili ya St. Peters Keberesi
- Magenge Secondary
- Soko la Riokindo
- Riokindo Boys
- Bouster
- Nyangeti Secondary
- Soko la Nyabitunwa
- Nyabiore Secondary
- Soko la Getenga
- Soko la Mageche
- Nyamesocho Secondary
- Soko la Geteni
- Mokomoni Secondary
- Jerusaremu
- Nyamodo
Nyeri
Kaunti ya Nyeri itakumbwa na kukatika kwa umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Maeneo yatakayoathirika ni:
- Soko la Kabiru-ini na maeneo ya karibu (Kabiru-ini Kwa
Gachau, Shule ya Upili ya Kabiru-ini, na Kiwanda cha Kahawa cha Kabiru-ini)
- Soko la Kiamariga
- Kiamariga Secondary School
- Kituo cha Polisi cha Kiamariga
- Shule ya Msingi ya Kianjau
- Kijiji cha Kianjau
- Milima ya Nyana
- Kijiji cha Njathe-ini
- Githiringo TBC
- Kijiji cha Gikiriri
- Kiamariga Hombe
- Booster za Safaricom na Airtel
Kirinyaga
Kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni, maeneo yafuatayo katika kaunti ya Kirinyaga yatakosa umeme:
- Chuo Kikuu cha Kirinyaga
- Kutus Old Town
- Kijiji cha Gitwe
- Soko la Karia
- Soko la Kiamwenja
- Shule ya Upili ya Ngaru
- Kiwanda cha Kahawa cha Karia
- Hosteli za Ngomongo na maeneo jirani
Tharaka Nithi
Umeme utakosekana katika kaunti ya Tharaka Nithi kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi jioni katika maeneo yafuatayo:
- Soko la Ndagani
- Seminari ya Fransaian
- St. Lucy
- High Mark
- Tumaini
- KwaJustin
Laikipia
Katika Laikipia, umeme utakatika kati ya saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni katika maeneo haya:
- Soko lote la Doldol
- Olkinyei
- Kiwanja Ndege
- Illipollei
- Kaimanjo
- Ol-Donyiro na wateja wa karibu