logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Boni Khalwale azungumzia kisa cha wabunge wanawake kupigana bungeni

Seneta Boni Khalwale aliweza kuzungumzia kisa cha wabunge wanawake kupigana mbele ya bunge machoni pa watu.

image
na Evans Omoto

Yanayojiri09 April 2025 - 12:04

Muhtasari


  • Seneta Boni alizungumzia kisa hicho akikitaja kama kilichochochewa na usemi wa uwakilishi wa theluthi mbili ya kina mama ya  uwakilishi katika  bunge la kitaifa.
Wabunge wa kike wakipigana katika bunge la Taifa

Seneta wa Kakamega Boni Khalwale amezungumzia kisa cha  wabunge wanawake kupigana katika majengo ya bunge machoni pa watu.

Seneta Boni alizungumzia kisa hicho akikitaja kama kilichochochewa na usemi wa uwakilishi wa theluthi mbili wa wanawake katika  bunge la kitaifa.

Alisema hayo akiashiria kuwa hilo lilikuwa ni jambo ambalo lilikuwa limepitilizwa na kutiwa chuki sana hadi kufikia kiiwangao cha wanawake  viongozi kuparuzana na kujivua  aibu mbele ya watu.

Katika video ambayo ilionekekana ikisambaa mitandaoni ilionyesha  wabunge  wa kike wawili wakipigana huku mmoja akionekana akiwatenganisha.

Kisa hicho kikiendelea kulisikika sauti kutoka mbali zikisema kuwa wawawache wapigane bila kupata msaada wa kuwatenganisha na ilionekana mbunge mmoja  akiwa  ameangushwa chini.

Mbunge mteule wa ODM Umulkheri Harun na Mbunge mwakilishi katika bunge la Afrika mashariki EALA Falhada Iman ndio waliokuwa wakipigana.

Katika video hiyo iliyowanasa iliweza kunasa sauti za  wabunge wengine  wakiwa karibu hapo sauti ilisikika ikisema kuwa wasitenganishewe  na badala yake waachwe waendelee kupigana.

Mbunge  mteule wa ODM Harun alisikitikia kisa hicho akikitaja kama kisa  cha aibu na ambacho anakijutia kuweza kuji husisha ndani yeye kama mzazi , kiongozi  na hasa mwanadini wa kiislamu.

Aliweza kusema kuwa alikuwa amechukua hatua  madhubuti kuweza kuripoti tukio hilo katika asasi husika huku akiomba msamaha na kusema kuwa kilikuwa kitendo cha aibu.

''Ni jambo la aibu sana  na ni kitendo ambacho sitaki kukizungumzia  kwa sasa ila ninaomba msamaha hasa kwa watu wote, hili jambo limenikoseshea heshima kama kiongozi, mama na mwanadini.

 Nitapeleka ripoti kwa asasi husika ili niripoti kwa maana  ni jambo ambalo linastahili kuangaziwa  na mamlaka husika ili kuwe na  uchunguzi wa  undani zaidi ila kwa sasa sina mengi ya kuzunguzia;; Harun aliweza kueleza.

Ni kisa  ambacho kwa nanma moja  au nyingine kiliweza kuwashusha hadhi wabunge wa kike kwa kuweza kujiaibisha mbele ya  halaiki ya wananchi na  ambao wanawawakilisha  hivyo kutaka kuangazia chanzo cha tukio hilo.

 Hata hivyo iwapo kuna jambao ambalo labda viongozi hawajakubaliana nalo ni vyema waweze kusulihisha mambo yao kwa usiri na  bungeni si mbele ya kamera tena kwa kupigana.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved