
Rais Ruto alikariri kwa kusema kuwa bima ya afya kwa wote alimaarufu UHC ilikuwa sawa na ya manufaa kwa wakenya.
Rais Ruto alisema hayo alipokuwa katika ikulu ya Nairobi siku ya Alihamisi 17,Aprili 2025 alipokuwa katika hafla ya kuwaapisha mawaziri walioteuliwa na waliopigwa na msasa na bunge la taifa na kupitishwa na bunge.
Rais alisisitiza kuwa taifa lilikuwa limejaribu kuendesha mfumo wa matibabu nchini Kenya akisema kuwa kwa serikali zilizopita zilijaribu kwa hatua kubwa kufanikisha mpango huo.
Rais alisema kuwa uongozi uliopita ulifanya bidii na jitihada kuhakikisha kuwa angalau mfumo huo unafanikiwa lakini kwa namna moja au nyingine malengo lengwa hayakuafikiwa.
Rais alisema kuwa aliyekuwa waziri wa Afya Charity Ngilu pamojana profesa Anyang' nyong'o walijaribu kaddri ya uwezo waxo kufanikisha mpan go wa bima ya afya kwa wote ikiwemo serikali ya Jubilee ila ufanisi ulikuwa finyu.
Rais alisema kwa wazi kuwa wakati sasa ulikuwa umewadia kwa kuweza kufanikisha mpango huo akisema kuwa mara hii itawezekana kwa kuwa ukuruba uliopo kati ya serikali ya Kenya kwanza pamoja na wanachama kutoka vyama vingine vya upinzani kwa serikali jumuishi .
Ruto alisema kuwa alikuwa na matumaini makubwa kuwa ushirikiano uliopo wa kisiasa kwa sasa ni ushirikiano amb ao utawezesha kila jambo na ahadi za serikali kutimia .
Kulingana na mujibu wa usemi wa Rais Ruto idadi ya watu au wakenya ambao walikuwa wakijiunga na bima hiyo ya UHC ilikuwa ya juu sana akisema kuwa jumla ya watu 50,000 huwa wanajisajili katika bima hiyo kwa siku kuashiria kuwa maendeleo makubwa yalikuwa yakionekana.
Vilevile Rais alisema kuwa alikuwa akipokea usemi kutoka kwa marafiki,wanajamii, watu aliosoma nao pamoja na wakenya kutoka matabaka mbalimbali kuhusu jinsi mpango wa UHC ulikuwa umewasaidia pakubwa kuweza kulipa bili za hospitalini na vilevile kuwapa wakati mwepesi kufanikisha na kuendeleza shughuli zao bila matata yoyote.
Rais alisema kuwa bima hiyo itawasidia wakenya wote kuweza kupata matibabu na wala si kama awali ambapo watu wachache ndio waliokuwa wakinufaika pakubwa huku wengi wakihangaika kwa kuuza mali zao kwa sababu ya matibabu.