

Akizungumza kwenye kituo kimoja cha redio humu nchini, Muturi aliendelea na kuleza kwamba rais Ruto ni mtu asiyeeleweka na ni watu wawili tofauti.
"Nadhani William Ruto ni mtu aina mbili tofauti, Ruto ambaye anaonekana kwa umma ni tofauti sana na yule anayekaa kwenye ikulu ya rais na kuifanya maamuzi. Na mtu kama huyo ni hatari. Nadhani kwamba william Ruto sio sahihi kuwa rais wa Kenya," alisema Mutruri.
"Hilo ndilo hitimisho langu na sina chuki na yeye, Nikiona rais akizungumza kwenye kikao cha mawaziri na anasema hataki kuona ufisadI kwa seriksali yake. Nashangaa huyu ni nani anaongea... yeye ni kiongozi wa ufisadi," aliendelea.
Waziri huyo wa zamani ameendelea na kueleza kuhusu mkataba wa Adani ambao walikuwa wamepewa idhini ya kumiliki uwanja wa ndege. Amesisitiza kwamba hakuna mkataba wa serikali ambao rais hufanya bila kufikiria atakachokipata yeye.
"Yeye ndie alikua nyuma ya Adani, Mshauri wake Adan Muhamed alinialika kwa mkutano na nikajua kila kitu kuhusu mpango huo. Ruto akija na shughuli yeyote inahusu kuunda pesa. Kuna wakati waliniletea mkataba wa MOU, kutoka wizara ya mazingira. Ilikuwa 1M US Dollars na wanataka hiyo pesa ipelekwe moja kwa moja kwa wizara ya mazingira bila kupitia hazina ya kitaifa," alieleza zaidi.
"Unaambiwa uende uweke sahihi kwa mkataba ukiwa kwa uwanja wa ndege, na ni rais anakupigia. Ni jambo la kushangaza sana kwamba tuko na Wiliam Ruto kama rais wa wa taifa la Kenya," alisema spika huyo wa zamani.
Rais Wlilliam Ruto alimfuta Muturi kazi huku akimtaja kama mtu asielewa kazi yake katika wizara zote mbili ambozo amefanya chini yake katika serikali ya Wlilliam Ruto.
"Nilikuwa na tatizo na Mwanasheria Mkuu aliyekuwepo hapo awali—alikuwa hana uwezo. Lakini sasa, nina mtu mwenye uwezo mkubwa katika nafasi hiyo, na nina hakika masuala ya Waqf yatatatuliwa ndani ya miezi michache," alisema Ruto.
Muturi hakusita kujibu tuhuma hizo, akisema kuwa madai ya Ruto hayakuwa ya kweli. Alieleza kuwa Sheria ya Waqf Na. 8 ya 2022 haielekezi kuanzishwa kwa "Mfuko wa Waqf wa Kiislamu" na kuongeza kuwa waqf ni mali ya hisani inayosimamiwa na Tume ya Waqf.