logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kennedy Rapudo Aeleza Kwa Nini Gavin, Mwanawe Amber Ray Hamuiti “Baba”

“Hapana, hujawahi niita babake. Kwa nini? Kwa sababu babake yuko hai. Na mara moja moja huwa wanakutana. Hivyo siwezi kumlazimisha kuniita baba."

image
na MOSES SAGWE

Burudani05 February 2025 - 13:33

Muhtasari


  • Kuhusu mtoto huyo kumuita baba, Rapudo alifichua kwamba muda wote huo, hujawahi fanya uthubutu wa kumuita ‘baba’.
  • Amber Ray kabla hajaolewa na Rapudo, alikuwa na mtoto wa kiume – Gavin – ambaye ni tineja.
  • Kwa upande mwingine, Rapudo kabla hajapata mtoto na Amber Ray miaka miwili iliyopita (Africana), alikuwa na watoto wawili kutoka kwa mahusiano yake ya awali.
caption

KENNEDY amezungumzia kina cha uhusiano wake na mwanawe mkewe, Amber Ray – Gavin.

Akizungumza na Dr Ofweneke kupitia podkasti yake, Rapudo alisema kwamba kuishi na kijana huyo tineja ni jambo la kujivunia akimtaja kama mtoto ambaye amelelewa katika maadili ya kupendeza.

“Gavin ni mvulana ambaye ana maadili mazuri sana, mamake kwa kweli amemlea na kumkuza katika njia nzuri na hatujawahi kuwa na matatizo,” Rapudo alisema.

Baba huyo wa watoto 3 alifichua kwamba mara kwa mara huwa wanazungumza ya kiume na Gavin.

“Huwa tunakuwa na mazungumzo ya kiume. Wakati ninaona kitu Fulani hakiko sawa au wakati nina changamoto kidogo huwa namwaambia, ‘unajua nini mbona tusitoke na gari?’… na huwa tunatoka na kuzungumza.”

“Halafu pia huwa namwambia jinsi ya kushughulikia baadhi ya masuala kama kuburuzwa mitandaoni, shuleni na wanafunzi wenzake na ni bwana mdogo mzuri sana.”

Kuhusu mtoto huyo kumuita baba, Rapudo alifichua kwamba muda wote huo, hujawahi fanya uthubutu wa kumuita ‘baba’.

“Hapana, hujawahi niita babake. Kwa nini? Kwa sababu babake yuko hai. Na mara moja moja huwa wanakutana. Hivyo siwezi kumlazimisha kuniita baba wakati babake mwenyewe yuko hai. Ni kesi sawia, huwa binti yangu anaita babake Gavin ‘baba’? hapana! Kwa sababu mimi kama baba niko hai na tunaheshimu hii mipaka yote na kila kitu kinaenda sambamba,” Rapudo alijieleza kwa maelezo ya kuridhisha.

Rapudo na Amber Ray ni wanandoa wachache ambao wana ufanisi mkubwa katika kuendesha familia mseto – kila mmoja akiwa na mtoto kutoka kwa uhusiano wa awali.

Amber Ray kabla hajaolewa na Rapudo, alikuwa na mtoto wa kiume – Gavin – ambaye ni tineja.

Kwa upande mwingine, Rapudo kabla hajapata mtoto na Amber Ray miaka miwili iliyopita (Africana), alikuwa na watoto wawili kutoka kwa mahusiano yake ya awali.

Alimueleza Ofweneke kwamba alipata mtoto wake wa kwanza, binti wa miaka 13 wakati alikuwa chuo kikuu mwaka wake wa pili.

Baadae pia alikuja kupata mtoto wake wa pili – mvulana, ambaye alilazimika kuelekea mahakamani miezi kadhaa iliyopita ili kupata idhini ya kuonana naye mara kwa mara baada ya kile alichokitaja kuwa mamake alikuwa mwenye drama nyingi.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved