

Muigizaji maarufu kutoka katika Taifa la Tanzania Wema Sepetu amefunguka na kuweka wazi kuhusu afia yake.
Kwenye mazungumzo na wanahabari, Sepetu amekiri kwamba amekuwa akiugua kutokana na makali ya Presha ambayo mara kwa mara imekuwa ikishuka hivyo kumuletea madhara.
"Mimi huwa nina presha. nina presha ya kushuka, mimi ni mgonjwa sana, mimi ni mbovu, sipo sawa. sina asilimia 100% ya afia yangu. kiufupi naumwa na madhara yako. hili la presha kushuka huwa linanitokea mara nyingi pamoja na uwoga," Sepetu alieleza.
Mwanadada huyo maarufu siku za awali aliwahi kupinga swala la kuwa na chanamoto za afya hasa baada ya kupoteza uzani wake ambao wafwasi wake walikuwa wameuzoea na kusema kwamba hali yake iko sawa.
" Nipo sawa, siuguwi kwa chochote. mwili ambao unaona leo ndo mwili ambao nimekuwa nikitafuta. Watu walinijuwa kama miss Tanzania nikiwa hivi mwembamba na uzani ukaja baadaye. Kisha wakanijua na wakaanza kusema nimekuwa mzito zaidi, nadhani utakuja muda ambapo watanizoea hivi," alieleza kwa kina wakati akikaidi madai ya kuwa na changamoto za kiafya.
Muigizaji huyo ambaye aliwahi kutwaa ushindi kwenye mapishano ya urembo mwaka 2006 kama "Miss Tanzania" pia amekuwa na tatizo la uzazi, jambo ambalo amelizungumzia mara kwa mara. Wakati wa mwisho akieleza kwamba tayari amekata tamaa kutokana na ndoto yake ya kupata mtoto.
Wema alieleza kuwa baada ya miaka mingi ya kujaribu kutafuta mtoto, alikuwa amefika mahali pa amani na kuikubali hali yake.
"Sijabarikiwa kupata mtoto na kiukweli kwa wakati huu hata mkiniambia mnanitakia heri, nimeshafika 35. Sitegemei kwamba nitashika mimba. nilikuwa na tamaa ya kupata mtoto, hata ile hamu, imefika wakati nimekata tamaa," alishiriki.
Licha ya changamoto, Wema huwa na imani yake kwamba kila kitu kinatokea kwa sababu. Aliwahi kusema hilo akirejelea kukosa mtoto.
"Nilijaribu kwa muda mrefu, lakini Mungu aliamua sikustahili. Huwezi kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Hakuna kitu kinachotokea kwa ajali katika dunia hii. Huwezi kujua kwa nini Mungu hakunipa mtoto wangu mwenyewe," aliongeza.



