
Muigizaji Wema Sepetu amefunguka na kueleza kwamba yeye kwenye suala la mapenzi, hupenda sana kwani hajui kumpenda mtu nusunusu.
Kwa upande wake pia ameeleza kwamba japo yeye hujitahidi kupenda huachwa na hili limemuumiza sana mara kwa mara.
"Mimi nikiwa niko na mtu kwenye mapenzi, siwezi kumupitilia kwa chochote, nitampa pendo langu lote, sababu mimi jambo la kupenda nusu nusu siwezani. ni kitu ambacho mwenyezi Mungu hajanijalia. Mimi nikipenda napendanga sana,' Alisema Wema Sepetu.
Muigizaji huyo Maarufu kutokea nchini Tanzania pia ameweka wazi kwamba anapomaliza kupenda kisha kutokee lolote la kuweka chuki huchukia sana katika asilimia sawa.
"Likija kwenye swala la kuchukia pia mimi huchukia sana," aliongeza Sepetu.
Mwanadada huyu ni mmoja kati warembo Mashuhuri katika taifa hilo ambao wamewahi kutoka kimapenzi na mwanamziki maarufu wa bongo, rais wa wasafi Diamond Platinumz ila wakaachana.
Sepetu pia aliwahi kuwa kwenye mahusiano ya mapenzi na nyota wa zamani wa kuigiza marehemu Steven Kanumba.
Mrembo huyu alijulikana sana wakati akiwa kwenye mapenzi na nyota hao wawili hasa mwanamziki Diamond
Mwanadada huyo kwa kuonesha kuumizwa na mapenzi sana hasa kutoka kwa mwanamziki Diamond ambaye pia ni bosi wa Wasafi aliwahi kuwachia filamu kuhusu mapenzi yao wawili.
Mwaka 2011, Wema Sepetu alitunga filamu kwa jina 'Superstar' ambapo alikuwa akisimulia maisha yake ya mapenzi na Diamond Platinum mmoja wa wasanii bora Tanzania
Sepetu kando na kuwa mwigizaji wa Tanzania ni mshindani wa urembo aliyejinyakulia taji la 'Miss Tanzania' mwaka 2006. Aliwakilisha nchi yake katika mashindano ya urembo ya 'Miss World 2006' nchini Poland.
Malkia huyo wa urembo wa Tanzania alizaliwa Septemba 28, 1988. Atatimiza umri wa miaka 37 mnamo Septemba 2025.
Siki za hivi karibuni Sepetu aliweka wazi kwamba amekata tamaa ya kupata mtoto kutokana na umri ambao anaamini kwamba unakwenda ila hajafanikiwa kupata mtoto.
Mwanadada huyo pia amepata mwingilio mkubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kumtaka Hamisa Mobeto kuondoka kwa ndoa yake iwapo atakosa amani siku chatu tu baada ya kufunga ndoa hio.
"Sina ushauri wowote kwa ajili yake. Naweza kumshauri tu aishi maisha yake. Anapaswa kuwa na furaha kwa sababu mimi simo katika ndoa yoyote. Kwa hiyo siwezi kumwambia, hilo ni jambo ambalo atajifunza. Ninachoweza kumwambia kama dada ni kwamba nataka awe na furaha. Kama anaona kuwa hana furaha yoyote, basi aondoke." Sepetu alimwelekezea Mobeso.

