
MKEWE mwinjilisti Guardian Angel, Esther Musila amewashauri watu kutotilia maanani sana kuchukiwa na binadamu wenzao, akitaja hiyo kuwa hali ya kawaida sana.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Musila
alidai kwamba mtu kuchukiwa na watu ni kawaida na wala halifai kukuingia katika
akili na kukupa Mawazo sana.
Ila alidai kwamba kama binadamu, unafaa kuwa
na wasiwasi mkubwa ikiwa utaanza kuchukiwa hadi na Wanyama, haswa mbwa.
Kulingana na Musila, chuki kutoka kwa
binadamu mwenzako ni kawaida sana kwani siku zote hasidi hana sababu lakini
chuki kutoka kwa mbwa ni jambo la mashaka ambalo linakupasa kujiita mkutano na
kujitathmini ulikobeta.
“Kama watu hawakupendi, si kawaida na
sawa. Lakini Kamba mbwa hawakupendi, basi huo ni wakati wa kujiita mkutano na
kujitathmini,” Musila alidai.
Lakini je, ni rahisi kupata mnyama aina ya
mbwa kumchukia binadamu?
Kwa mujibu wa Rover.com, Mbwa hupenda
wanadamu kutokana na mchanganyiko wa mambo, ikiwa ni pamoja na historia yao ya
mabadiliko, akili ya kijamii, na uimarishaji mzuri wanaopokea kutokana na
mwingiliano wa binadamu.
Mbwa wamefugwa kwa maelfu ya miaka,
wakibadilika na kuunda vifungo vikali na wanadamu, na wana uwezo wa kuelewa na
kukabiliana na hisia za kibinadamu na ishara za kijamii.
Wakati mbwa huingiliana na watu na kuwa na
uzoefu mzuri, hupata kasi ya kujisikia vizuri ya dopamine, hivyo si rahisi
kupata mbwa akimchukia binadamu.
Mbwa hupenda kulamba. Wakati mbwa anakulamba,
anakubusu. Kumbusu ni ishara ya ulimwengu wote ya mapenzi, hata kati ya mbwa!
Kulamba kwa mbwa pia ni tabia ya kutafuta umakini. Kwa hivyo ikiwa mbwa wako
anakulamba, anaweza kuwa anakuuliza wakati wa kucheza, kubembeleza, au kipenzi.
Mbwa wako anapokujia na kuegemea uzani wake
kamili dhidi ya miguu yako, anakuonyesha kwamba anakuamini na kukupenda kabisa.
Kwa maelezo haya, ni bayana kwamba si kawaida
kwa mbwa kumchukia binadamu na ikitokea anamchukia, basi kuna suala kuu tena la
dharura ambalo mtu unafaa kujiita mkutano.