logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamume amuua mkewe na kutoroka Ngong

Amesema  polisi wa Ngong kwa ushirikiano na DCI wanatarajiwa kuanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo .

image
na Radio Jambo

Dakia-udaku08 December 2020 - 12:25

Muhtasari


  •  Amesema  polisi wa Ngong kwa ushirikiano na DCI wanatarajiwa kuanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo .
  •  Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya kajiado  Kaskazini Rashid Mohamed  amethibitisha tukipo hilo akisema  mwanamke huyo alikimbizwa katika hospitali ya zama zama ambako aliaga dunia .

 

Crime scene

 Polisi katika  eneo la Kibiko huko Ngong wanamsaka mwanamme mmoja aliyemuua mkewe na kisha kutoroka

 Tukio hilo limefanyika katika kituo cha kibiashara cha  Oloolua ambapo mshukiowa alimfuata mkewe hadi katika sehemu yake yabiashara na kisha kumuua kwa kumdunga kisu .

 Jamaa huyo aliyetambuliwa kama ‘Mutembeli’  aliingia katika sehemu ya biashara ya mke wake na kuanza kugombana naye mwendo wa saa tano asubuhi . Jirani yao mmoja  Henry Kinyanjui amesema  wawili hao wamekuwa wakilumbana kila mara .

‘wamekuwa wakitofautiana l;akini sikujua kwamba shambulizi la leo litasababiusha kifo ‘ amesema Kinyanjui .

 Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya kajiado  Kaskazini Rashid Mohamed  amethibitisha tukipo hilo akisema  mwanamke huyo alikimbizwa katika hospitali ya zama zama ambako aliaga dunia .

 “ OCS wangu anakusanya maelezo  na akitayarisha ripoti  basi nitawaarifu kuhusu kilichofanyika’ amesema Mohammed .

 Amesema  polisi wa Ngong kwa ushirikiano na DCI wanatarajiwa kuanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo .

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved