logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwimbaji Mbilikimo Grand P Anataka Kupata Mapacha na Mpenziwe Mpya Mariame

Bwenyenye huyo kutoka Guinea amesema kwamba Mariame ni mama wa baadaye wa mapacha wake.

image
na Samuel Mainajournalist

Dakia-udaku26 February 2025 - 08:31

Muhtasari


  • Katika moja ya machapisho yake, ambapo alijigamba kuhusu mpenziwe, Grand P alishiriki video ya Mariame na kumuita mwanamke mwenye bahati.
  • Kauli yake inaonekana kuashiria matamanio ya mwimbaji huyo ya kupata mapacha na mpenzi wake mpya katika siku za usoni.

Grand P na mpenziwe Mariame

Mwanamuziki na mshawishi wa mitandaoni mashuhuri wa Guinea, Moussa Sandiana Kaba, almaarufu kama Grand P, amedokeza nia yake ya kupata mapacha na mpenzi wake mpya.

Msanii huyo, anayejulikana kwa mwonekano wake wa kipekee, alimtambulisha mpenzi wake mpya, Mariame Kaba, takriban wiki tatu zilizopita. Tangu wakati huo, amekuwa akijivunia mahusiano yao na kumtangaza kwa mashabiki wake kwa fahari. Kinachowashangaza wengi kuhusu mpenzi wake mpya ni maumbile yake madogo ya kipekee, ambayo karibu yanafanana na yake.

Katika moja ya machapisho yake kwenye mitandao ya kijamii, ambapo alikuwa akijigamba kuhusu mpenzi wake, Grand P alishiriki video ya Mariame na kumuita mwanamke mwenye bahati.

Msanii huyo mbilikimo alisema zaidi kuwa Mariame ni mama wa baadaye wa mapacha wake.

"Mwanamke mwenye bahati, mama wa baadaye wa mapacha wa Kaba," aliandika Grand P chini ya video ya Mariame ambayo alichapisha Facebook.

Kauli hiyo inaonekana kuashiria matamanio ya mwimbaji huyo ya kupata mapacha na mpenzi wake mpya katika siku za usoni.

Wiki iliyopita, Grand P alilalamika baada ya kupokea kauli za kejeli kwamba mpenzi wake mpya ni mtoto sana kwake kutoka kwa wale waliokuwa wakimcheka kwamba mpenziwe wa zamani ,mwanasosholaiti Eudoxie Yao, hakuwa size yake.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Grand P alisema kwamba hajui watu wenye chuki huwa wanataka nini kwani wao ndio walikuwa wanamcheka kuwa Eudoxie Yao ni mkubwa sana kwake na sasa baada ya kupata wanayetoshana, bado watu wameibuka na kejeli kwamba ameoa mtoto.

“Ufike wakati mkome sasa watu wangu, wakati nilipost Jirani yangu (Eudoxie Yao), mliongea sana hadi mkachoka mkisema sio size yangu. Nilikubali ukosoaji wenu. Sasa nimepata ambaye ni size yangu na mumeleta kauli eti nimeoa mtoto. Watu wenye chuki sana nyinyi... kueni na siku njema,” Grand P alisema.

Katika picha hiyo, alikuwa ameshikana na mpenzi wake mpya ambaye alimtambulisha siku ya wapendanao kwa jina Mariame Kaba.

Kijana huyo amekuwa katika miaka ya nyuma kwenye uhusiano na sosholaiti wa Ivory Coast Eudoxie Yao ambaye ana umbile kubwa maradufu kumliko Grand P.

Uhusiano wake na Yao ulionekana kutumbukia mchangani mapema 2023 ambapio kufikia Aprili, alitangaza kuingia katika penzi la mwanadada mwingine aliyeitwa kwa jina Yubai Zhang.

Balozi huyo wa Guinea nchini Mali alikatisha mahusiano yake na mwanamitindo Yao mwaka wa 2021 baada ya kuwa kwenye mahusiano na mwanamitindo huyo kwa takriban miaka mitatu.

Wawili hao walitangaza kukuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi mwaka wa 2020 baada ya kuchapisha picha wakiwa pamoja.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved