
KISANGA cha karne kilishuhudiwa katikati mwa mji wa Kericho baada ya mwendesha bodaboda mmoja kutokea akiwa anaendesha pikipiki yake akiwa uchi wa hayawini.
Katika kisa hicho ambacho kilinaswa kwenye video na kupakiwa
kwenye mitandao ya kijamii, jamaa huyo aliwashangaza wenzake ambao mwanzo
walionekana kuogopa kumkaribia wakidhani amepandwa na maruani ya kwake.
Baada ya kuonekana kuchanganyikiwa zaidi, wanabodaboda
wenzake walimzunguka na kumsimamisha huku wakifanya juhudi za kumsitiri kwa
angalau na nguo, jambo ambalo alionekana kutolitaka kamwe.
Baadae, jamaa huyo alifanikiwa kukwepa kutoka kwa kundi la
wanabodaboda wenzake waliomzunguka na kutokomea, akiwaacha wengi katika hali ya
mshangao wasijue kama jamaa huyo alikuwa amekumbwa na tatizo la kiakili au
alikuwa anaigiza tu kuzua kioja.
Video hiyo ilichapishwa kwenye Facebook na mtumizi mmoja kwa
jina Trch Collo na kuvutia maoni ainati.
@Glenda Glenz: “Mbona nacheka...Na mbona walicrowd wangeaja
apigwe picha vizuri...si alitafuta content ya kutrend.”
@Fai Faith: “Na ameguzwa kidogo akakimbia, he knows what he
is doing sio wazimu. Mwaka karibu iishe kama sijaona kamjulz.”
@Chemutai Kirwa: “Kuomoka hii Kenya inataka ukue wazimu ndio
utrend.”
Tazama video hiyo hapa: