Polisi katika eneo la Kibiko huko Ngong wanamsaka mwanamme mmoja aliyemuua mkewe na kisha kutoroka
Tukio hilo limefanyika katika kituo cha kibiashara cha Oloolua ambapo mshukiowa alimfuata mkewe hadi katika sehemu yake yabiashara na kisha kumuua kwa kumdunga kisu .
Jamaa huyo aliyetambuliwa kama ‘Mutembeli’ aliingia katika sehemu ya biashara ya mke wake na kuanza kugombana naye mwendo wa saa tano asubuhi . Jirani yao mmoja Henry Kinyanjui amesema wawili hao wamekuwa wakilumbana kila mara .
‘wamekuwa wakitofautiana l;akini sikujua kwamba shambulizi la leo litasababiusha kifo ‘ amesema Kinyanjui .
Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya kajiado Kaskazini Rashid Mohamed amethibitisha tukipo hilo akisema mwanamke huyo alikimbizwa katika hospitali ya zama zama ambako aliaga dunia .
“ OCS wangu anakusanya maelezo na akitayarisha ripoti basi nitawaarifu kuhusu kilichofanyika’ amesema Mohammed .
Amesema polisi wa Ngong kwa ushirikiano na DCI wanatarajiwa kuanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo .



