logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nyahunyo:Mume wangu amekuwa akila chakula cha mtoto ilhali hanunui

Kulingana na mwanamke huyo, mumewe amekuwa akila chakula cha mtoto wao ambaye ana miezi tisa

image
na Radio Jambo

Habari07 July 2021 - 14:11

Muhtasari


  • Mume wangu amekuwa akila chakula cha mtoto ilhali hanunui
  • Kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa na tabia za kusikitisha na hata kukosea jamii bila ya kujali matokeo yake

Je una mtu ambaye ana tabia mbovu au amekosea jamii, haya basi husitie shaka kwani unaweza mleta katika kipindi cha nyahunyo ili atolewe makosa yake.

Kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa na tabia za kusikitisha na hata kukosea jamii bila ya kujali matokeo yake.

Mwanamke mmoja kutoka kaunti ya Nairobi alitaka mumewe atolewe makosa baada ya kuwa na tabia ya kula chakula cha mtoto wake.

Kulingana na mwanamke huyo, mumewe amekuwa akila chakula cha mtoto wao ambaye ana miezi tisa

"Mume wangu amekuwa akila chakula cha mtoto wetu, nikimuuliza kwanini anafanya hivyo ananiambia kwamba anataka kuonja

Pia amekuwa akiamka usiku na kulamba asali ya mtoto, anasema kwamba anataka kujua kama ni kali au la

Nataka apewe nyahunyi awache tabia hiyo, kwa maana hanunui chakula ya mtoto lakini anakula hayo yamekuwa mazoea yake," Alisimulia mwanamke.

Je mwanamume huyo alihitaji kupewa nyahunyo au la?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved