

Kiongozi wa taifa daktari William Ruto leo Jumanne Februari 4, 2025 alizuru kaunti ya Mandera ajenda kuu ikiwa ni kuangazia, kuzindua na kutangaza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Rais William Ruto akizungumza akiwa katika uga wa Moi kule Mandera akiwa ameandamana na naibu wake wa raisi Profesa Kithure Kindiki, waziri wa mazingira Aden Duale pamoja na katibu wa usalama wa ndani Raymond Omolo rais aliwahutubia wakazi wa Mandera kwanza kwa kuwashukuru kwa kuwa waaaminifu na kuunga serikali mkono kikamilifu.
Rais William Ruto alianza hotuba yake kwa kutangaza mipango na mikakati ya maendeleo ya taifa akisisitiza kuhusu umoja na ushirikiano wa wananchi na viongozi ambao utawezesha maendeleo nchini. Rais alitangaza ukarabati na kutengenezwa kwa barabara mbalimbali miradi ambayo amewahakikishia wakazi wa Mandera kuwa barabara zote zitatengenezwa na kutamatika kwa wakati ili kurahihisha usafiri.
Ruto vilevile alizungumzia kuhusu miradi ya nguvu za umeme ambayo alitangaza kuwa serikali itahakikisha kuwa kila mtu anapata umeme ili kuhakikisha kuwa wananchi wa Mandrea pamoja na ukanda wa kasikazini mshariki Ya Kenya wananufaika pakubwa na miradi ya serikali bila mtu yeyote kusazwa.
Rais william Ruto aligusia sana mpango mzima wa usalama upande huo wa kazikazini ya kenya kwa kuhakikisha kuwa usalama unatiliwa mkazo na kuwa kipau mbele kwa kuhakiksha kuwa usalama unaimarishwa na hakuna mtu yeyote ataishi kwa kuhofia maisha yake.Hii inajiri siku moja baada ya magaidi kuwateka nyara machifu maeneo hayo.
Rais Ruto katika maelezo yake aliwarai wakazi wa Mandera wakumbatie mpango wa kuchanja mifugo kwa kuhakikisha kuwa mifugo wao wanachanjwa ipavyo ili kuepuka maradhi kwa kufanya hivyo watakuwa wanaimarisha viwango vya soko la nyama katika viwango vya kimataifa na nyumbani hata hivyo Ruto aliwahakikishia wafugaji waliopoteza mifugo yao kwa sababu ya kiangazi kuwa serikali itawafidia.
Rais william Ruto aliendeleza msururu wa miradi mbalimbali akizungumzia suala la elimu akisema kuwa kila mwaka serikali hutenga mabilioni ya fedha kwa idara ya elimu ili watoto wasome kwa hivyo yafaa kuwe na idadi kubwa ya wanafuzi ambao wanajiunga na taasisi za elimu ili kuhakikisha kuwa elimu inatolewa kwa usawa na kwa kila mmoja.
Vilevile rais aligusia swala la wakazi wa Mandera kupokea vitambulisho na stakabadhi muhimu kama pasipoti pasi kuangazia dini,ngozi au ukabila rais akiwahakikishia wananchi kuwa maendeleo ya taifa hayatabagua maeneo yoyote nchini akiwataka viongozi kufanya kazi kwa pamoja ili kutimiza na kuafikia viwango vya maendeleo kote nchini.