
WAZIRI wa utumishi wa umma, Justin Muturi ametaja sababu ambayo inamfanya hawezi hata kidogo kuwa na fikira za kujiuzulu kutoka kwa serikali ya Kenya Kwanza.
Akizungumza Jumatano katika kikao cha JKL
kwenye runinga ya Citizen, Muturi ambaye amekuwa mwiba Mchungu kwenye kitovu
cha serikali inayoongozwa na rais William Ruto alisisitiza kwamba hana mpango
wa kujiuzulu.
Spika huyo wa zamani alisema kwamba
ameketi kikato katika serikali ya Kenya kwanza nah ana mpango wa kujiuzulu kwa
kuwa alishiriki kikamilifu katika kampeni za uchaguzi mkuu 2022 kumpigia debe
Ruto kuwa rais.
“Mimi bado niko kwa serikali kwa
sababu kama mnavyojua bado niko kwenye ule muungano na pili ni kwamba
nilishiriki kikamilifu katika kampeni za Kenya Kwanza kuelekea uchaguzi mkuu wa
2022. Na hivyo niko kikamilifu katika haki zangu za kimuungano kuwa ndani ya
serikali,” Muturi alisema.
Kuhusu chama cha DP ambacho alikuwa
anakiongoza kabla ya kuteuliwa kama mwanasheria mkuu na baadae Waziri wa
utumishi wa umma, kuandika barua rasmi wakitaka kujiondoa katika serikali,
Muturi alisema kwamba huo ni uamuzi wa chama nah ana mkono katika uamuzi huo.
Muturi aliweka wazi kwamba kabla ya
kuteuliwa kutumikia serikali ya Kenya Kwanza, alijiuzulu kama mwenyekiti wa
chama hicho na kwamba barua ya kutaka kujiondoa kwenye Kenya Kwanza aliiona tu
kama Mkenya mwingine yeyote.
Waziri huyo alisisitiza kwamba uamuzi wa
chama ulifanywa na wakuu ndani ya chama hicho, akisema kwamba hakuna mwingilio
wowote kutoka upande wake.
Muturi amekuwa akionekana kuipinga
serikali anayoihudumia haswa baada ya mwanawe kuwa miongoni mwa waliotekwa
nyara na vyombo vya dola wakati wa kilele cha maandamano ya Gen Z mwaka jana.
Mara si moja, Waziri huyo ameitisha
mikutano na vyombo vya Habari kukashifu jinsi baadhi ya idara za serikali haswa
katika masuala ya usalama zinavyoendeshwa, akilaani vikali ongezeko la utekaji
nyara na kamata-kamata ambazo zimekuwa zikiendeshwa na maafisa wa usalama.
Katika mazungumzo hayo, Muturi aliweka
wazi kwamba tangu aonekane kuanza kuipinga serikali anayoihudumua, hajawahi
hudhuria kikao chochote cha baraza la mawaziri, ikiwemo kikao cha juzi
kilichofanyika katika ikulu ya Nairobi.