Rais William Ruto amewataka viongozi wa upinzani kuwasilisha ajenda zao za maendeleo kwa wananchi wa Kenya badala ya kuchochea chuki na uvunjifu wa sheria.
Akizungumza siku ya Jumamosi, Rais Ruto alisema kwamba huo ndio mwelekeo sahihi ambao upinzani unapaswa kuchukua badala ya kuchochea chuki na vurugu.
Rais huyo alikuwa tayari amewakosoa viongozi wa upinzani kwa kuchangia chuki na ukabila ilhali maisha ya watu yanapotea na mali pamoja na biashara kuharibiwa wakati wa maandamano.
Ruto alisisitiza kuwa hali hiyo lazima ikomeshwe kwa njia yoyote ile, huku akiwaonya wale wanaohusika na wimbi la hivi majuzi la uharibifu wa mali wakati wa maandamano kote nchini, akisema kuwa serikali itawafuatilia bila kujali nafasi yao katika jamii.
Alisisitiza kuwa serikali yake itakuwa imara dhidi ya viongozi wanaowatumia vijana kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa.
"Upinzani lazima uwasilishe ajenda yao ya maendeleo kwa Wakenya badala ya kuchochea uvunjifu wa sheria, chuki na ukabila. Tutasimama imara dhidi ya viongozi wa aina hiyo wanaowatumia vijana kwa ajili ya kuokoa maisha yao ya kisiasa yanayodorora,” Ruto alisema kupitia ukurasa wake wa X.
Rais huyo alikuwa tayari amewakosoa viongozi wa upinzani kwa kuchangia chuki na ukabila ilhali maisha ya watu yanapotea na mali pamoja na biashara kuharibiwa wakati wa maandamano.
Ruto alisisitiza kuwa hali hiyo lazima ikomeshwe kwa njia yoyote ile, huku akiwaonya wale wanaohusika na wimbi la hivi majuzi la uharibifu wa mali wakati wa maandamano kote nchini, akisema kuwa serikali itawafuatilia bila kujali nafasi yao katika jamii.
“Wote wanaotaka kuleta vurugu nchini Kenya, tutawaadhibu. Haiwezekani watu waende kuharibu mali ya wengine, kuchoma biashara za watu, vifo vitokee halafu walete siasa za kijinga, chuki na ukabila. Nimesema haya lazima yakome nchini Kenya,” alisema.
Kwa mujibu wa Rais Ruto, uharibifu ulioonekana katika miji mbalimbali nchini haukutokea kwa bahati mbaya bali ulikuwa umeandaliwa.
Alisisitiza kuwa utawala wa sheria lazima utamalaki ili kulinda maisha, riziki za wananchi, na miundombinu ya umma.
“Wale wote mlioshiriki katika uharibifu wa mali katika miji yetu, iwe ni Nyeri, Murang’a, Meru, Embu au Kirinyaga, tutawafuata,” alisema.
“Haswa waliopanga vurugu hizi. Msituambie ni mateso ya kisiasa. Hali ni kama ilivyo.”
Ruto: Uchumi wa Kenya Umo Miongoni mwa Sita Bora Barani Afrika
Aliyasema hayo wakati wa toleo la 9 la Mpango Jumuishi wa Uhifadhi wa Mazingira wa Kaptagat, Simotwo, Kaunti ya Elgeyo Marakwet.
Ruto pia aliwataka viongozi wa kisiasa na kidini waache kuwachochea vijana kuingia katika vurugu, uhalifu na uharibifu wa mali.
“Lazima tusimame kama taifa na tujiulize, hivi kweli hiki ndicho tunachotaka kufanya?”