logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Polisi wawakamata washukiwa Wanane waliohusika katika kuwaibia Raia katika barabara kuu ya Thika

Matukio hayo ya wizi yalijiri mnamo Machi 11,2025 baada ya Rais Ruto Kuzuru eneo la Mathare kutumia barabara kuu ya Thika

image
na Evans Omoto

Yanayojiri14 March 2025 - 10:00

Muhtasari


  • Polisi walianzisha msako mkali kufuatia msururu  wa wizi katika Barabara kuu  ya Thika mnamo Machi 11,2025 baada ya kundi la vijana kuvamia magari  na wasafiri baada ya mkutano wa Rais Ruto.
  • Katika taarifa iliyosomwa Alhamisi Machi 13,2025 kutoka kwa idara ya  upelelezi wa makosa ya Jinai DCI ilidhibitisha kuwa angalau  watu wanane walikamatwa kutokana na tukio hilo.

Washukiwa waliokamatwa na polisi

Polisi walianzisha msako mkali kufuatia msururu  wa wizi katika Barabara kuu  ya Thika mnamo Machi 11,2025 baada ya kundi la vijana kuvamia magari  na wasafiri baada ya mkutano wa Rais Ruto.

Katika taarifa iliyosomwa Alhamisi Machi 13,2025 kutoka kwa idara ya  upelelezi wa makosa ya Jinai DCI ilidhibitisha kuwa angalau  watu wanane walikamatwa kutokana na tukio hilo.

‘Kwa kujibu madai na tetesi kutokana na matukio  ya uvamizi na wizi yaliyotekelezwa na watu waliolenga  watu wasio na hatia  katika Barabara kuu ya Thika  mnamo Machi 11,2025 , Maafisa wa polisi wameanzisha  uchunguzi  wa kuwatambua wahalifu hao wote waliosababisha vitendo hivyo vyote vya uchama’  DCI  ilieleza.

DCI iliweza kumtambua mshukiwa mmoja kwa Jina Junior Odinga aliyekuwa amejihami kwa kisu  alipovamia raia mmoja na kumuibia simu aina ya Oppo A77S  iliyotoka shilingi elifu ishirini na nane 28,000.

‘’Oginga alikamatwa katika Barabara kuu ya Thika na kupelekwa  katika kituo cha polisi cha Pangani  taarifa ilieleza''.

Washukiwa wengine saba waliweza kukamatwa kutokana na msako mkali ulioendeshwa na maafisa wa polisi, waliokamatwa ni Jared Nyanza,Darlin Lande,Daniel Okombe,Mike Robert,Elvis Otieno,Reagan Omondi na Mathenge Gathiri hao walikamatwa kwa kuwaibia wapita njia katika eneo la Mathare mtaa wa 4( Mathare Area 4).

Washukiwa hao waliweza kupelekwa katika kituo cha polisi cha Muthaiga DCI ilieleza.Polisi waliweza kupata shati saba mpya ambazo zilikisiwa ziliibiwa kutoka kwa waathiriwa,DCI ilieleza kuwa washukiwa wote waliweza kukamatwa na kufikishwa katika vituo vya polisi ili kuandikisha taarifa.

Pikipiki nyingi zilionekana siku ya Jumanne Adhuhuri zilizowashutua wasafiri na watumizi wa Barabara kwa kusababisha hali ya wasiwasi na sintofahamu miongoni mwa wananchi.

Katika Video zilizoonekana katika  mitandao ya kijamii zilionyesha vijana  wengi  wakifunga sehemu za Barabara, kuwalazimisha wapitanjia kuwapa walivyokuwa wamebeba Pamoja na kuwaibia waliokuwa ndani ya magari ya binafsi.

Walekwa wa matukio hayo walipata wakati  mgumu kuweza kujinasua kutoka kwa wahuni hao huku tahadhari ya kutotumia Barabara hiyo ikisambazwa mitandaoni kuwaonya wananchi kutotumia Barabara hiyo.

’Kwa sasa wasafiri muepuke kutumia Barabara kuu  ya Thika katika mpitio wa Barabara ya wasafiri wa miguu ya  KCA kuna kundi la Vijana amabalo linawaibia watu na hata kuingia kwenye magari ya umma Huduma ya polisi kwa umma tunataka  usaidizi wenu maelezo kutoka kwa Sikika Usalama Kwa Barabara(Sikika Road Safety) yalichapishwa katika ukurasa wao wa Facebook mnamo Machi 11,2025’’.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved