
Rais Willam Ruto amezindua mpango maalum unaojulikana kama shirika plan kwa ajili ya Wakimbizi nchini.
Ni mpango maalum ambao unalenga kuwasaidia na kuwakubali wakimbizi katika jamii pana ya Wakenya ili kuweza kutambuliwa na kuheshimiwa sana katika taifa.
Kenya ilianzisha mpango wa kuwakaribisha wakimbizi nchini mnamo mwaka wa 1980 kutoka kwa mataifa jirani kutokana na vita katika mataifa yao.
Mnamo mwaka wa 1991 hadi 1992 Kenya iliweza kuwapokea wakimbizi kutoka taifa la Somalia.
Taifa la Kenya lina Kambi mbili kuu za kuweza kuwahifanyi na kuwapokea wakimbizi wa ndani kwa ndani au kutoka nje ya mataifa mengine kambi ya Daadab na kambi ya Kakuma.
Kuna kambi ya Daadab ambayo ilianzishwa mwaka wa 1991 ambayo iliweza kuwapokea wakimbizi zaidi ya 420,000 kutoka taifa la Somalia kutokana na kuzuka kwa vita katika taifa hilo la Somalia ambapo kulizuka machafuko ya vita kati ya serikali ikiongozwa na Syyad Bare na waasi mwaka wa 1992.
Mnamo mwaka wa 2011 taifa la Kenya liliweza kupokea wakimbizi wengine 130,000 kutoka taifa la Sudan Kusini hio ni kutokana na machafuko ya vita vikali vilivyoshuhudiwa kati ya rais Salvakir na Riek Machari ambapo watu wengi waliweza kuuwawa na wengine kupoteza makao hivyo kukimbilia mataifa jirani kwa ajili ya usalama wao.
Kenya Pia ina kambi nyingine ya Wakimbizi ambayo inaitwa Kakuma ambayo mara nyingi hupokea wakimbizi kutoka taifa la Uhabeshi( Ethiopia)
Kenya imekuwa mshiriki mkuu wa kupokea na kuwasaidia wakimbizi kwa kile ambacho kinaonekana kuwa ni taifa lenye amani na lenye sheria na mikakati bainifiu ya kuhakikisha kuwa usalama wa wakimbizi unazingatiwa ipasavyo kwa ajili ya kuwa kwa amani na umoja.
Kenya huweza kuwapokea wakimbizi kutoka mataifa ya Somalia, Sudan, Demokrasia ya Kongona na taifa la Burundii.
Chini ya kifuchiu cha sheria cha mwaka wa 2011 sheria hiyo imewapa uhuru wa makao na kuishi katika taifa la kenya kwa kupata haki zote za kimsingi na kuweza kujumuika kama raia wengine na kupata haki za kimsingi kutoka katika taifa la Kenya.
Kwa hivyo rais kuanzisha mchakato huo ni njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa wakimbizi wanaishi kama wakenya wengine na kufaidi kwa miradi ya serikali na hata vilevile kuweza kukaribisha misaada kutoka kwa mataifa mengine ambayo yana ari ya kusaidia kukuza umoja na ubinadamu.