
Manaibu Gavana wasisitiza kutengewa bajeti yao kando ili kuendeleza kamati mbalimbali katika Kaunti.
Manaibu wa magavana walielendeleza wito wa kutaka kupewa bajeti yao katika masuala ya uongozi.
Walizungumuzia swala hilo kwenye bunge la Seneti kuhusu masuala ya ugatuzi wakiongozwa na mwenyekiti wao Reuben Kamuri.
Manaibu magavana
hao waliweza kusema kuwa wana ujuzi na uwezo wa kuweza kutekeleza majukumu mengine
ya uongozi katika serikali za kaunti na kuimarisha uongozi
mwema.
Waliweza kusema kuwa
kwa mara nyingi wamekuwa wakisalia kupangwa na magavana wao bila kupewa
majukumu maalum ya kufanya kazi.
Waliweza kusema kuwa wangependa Katiba iweze kubadilishwa
ili kuwe na bajeti yao maalum Pamoja na
kazi zao ambazo zinatambulikana
kikatiba.
Walisema kuwa kwa mara nyingi magavana wamekuwa wakiwatumia
kutafuta kura baaada ya hapo wanawatelekeza na kuwawacha
katika hali ngumu bila wao kujua hatima
yao ya uongozi.
Usemi wa uliweza
kuungwa mkono na baadhi ya maseneta kama
Mpuri Aburi wa Meru waliosemkuwa kwa
hakika manaibau magavana wamekuwa wakipitia hali ngumu
katika wakati wao wa uongozi kwa kukosa kazi mwafaka na inayotambulikana kisheria.
‘’Ni wazi kuhusu kile mbacho manaibu wa magavana wanastahili kuwa
wakifanya lakini ni jambo la kusikitisha kuona magavana
hao wanafanya kazi katika huruma ya Magavana jambo ambalo ni la kusikitisha sana inasitahili sheria zibadilishwe ili tuwe na kazi
maalumu na bajeti maalum ya
kutekeleza baadhi ya miradi
mbalimbali katika serikali za
kaunti’’. Ruben Kamuri mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu ugatuzi alisema.
‘’ Ninaunga mkono pendekezo hilo la manaibu magavana kupewa bajeti yao ili waweze pia
kuendeleza baadhi ya sera za maendeleo katika uongozi wa Kaunti mwanzo
hawa viongozi wana ujuzi na tajiriba pana kuhusu uongozi’’ Mpuri Aburi alisema
Kwa mara si moja kumeshuhudiwa mizozo na mwingiliano wa masuala ya uongozi kati ya magavana na manaibu wao kuhusu uongozi jambo ambalo huisha kusababisha kukuwa na miswada ya kung’atua magavana uongozini jambo ambalo huleta vita vya kimaslahi.