

TIKTOKER Obidan Dela kwa mara ya kwanza amefunguka kwa nini anajitambua kama mume wa wanawake waliofiwa na waume zao, wale walioachwa na baba watoto wao na kina ajuza.
Akizungumza kwenye podikasti ya Mwende Macharia, Dela alisema
kwamba aliamua kukumbatia jina hilo baada ya TikTokers wenzake kuanza kumuita
hivyo kimchezo.
Kwa mujibu wa Dela, aliona kujiita ‘mume wa waja, bibi na
mama wasio na waume’ si vibaya kwani pia aligundua wengi wa watu ambao walikuwa
wanamlilia kwa misaada ya kila aina ni watu kutoka matabaka hayo matatu.
“Mimi ni mume wa wajane,
single moms na pia bwana wa ajuza wote. Na hii ilikuja kutoka kwao kwa sababu
mimi ndio hutoa jukwaa pekee la kuwasaidia watu kwenye TikTok. Sasa hivi hata
usikie kama uko na shida umefungiwa nyumba, ukija kwa Obidan Dela utapata
msaada,” alisema.
Alisisitiza kwamba watu kumuita mume wa wajane ni ishara ya
kusifia jinsi anavyowasaidia watu wasiojiweza.
“Kwangu mimi wakiniita
mume wa wajane ni njia ya kuni’appreciate. Mimi ndiye mtu pekee ambaye naweza
ingia TikTok Live nikose kujisaidia na nisaidie watu. Mimi huwa sifanyi mzaha
TikTok,” Dela alisema huku akitetea kusaidia kwake watu kutokana na
yale maisha ambayo alikulia.
TikToker huyo pia aliweza kuzungumzia kuhusu uhusiano wake na
Esther, nyanya yake aliyekuwa TikToker Brian Chira.
Dela alisema kwamba anampenda sana ‘shosho wa Chira’ huku
akitetea jinsi alimpeleka katika mgahawa ghali siku ya wapendanao kufurahisha
maisha.
“Mimi ndio nilikuwa mtu
wa kwanza kuleta shosho wa Chira TikTok. Watu walikuwa wananiita ‘kijana wa
shosho’ kwa sababu ya kusimama na yeye.”
“Mimi na Shosho wa Chira
ni mapenzi tu, unajua tunafanya out of love. Shosho anastahili kupendwa kwa
sababu hujawahi pendwa. Hata ile kumpeleka mgahawani afurahie Valentine ilikuwa
ni surprise sana. Unajua hujawahi nunuliwa nguo…unajua kitu kimoja kimoja
kuhusu Valentine ni kwamba si lazima umpende mtu ndio umfanyie kitu, unaweza
surprise mzazi wako…ni mwezi wa mapenzi na unaweza onyesha mapenzi hata kwa
mbwa wako, jirani, kakako…hiyo ndio maana ya Valentine,” Dela alitetea uhusiano
wake na Shosho.






© Radio Jambo 2024. All rights reserved