
CHARLIE Jones, kijana mdogo ambaye amekuwa akitajwa kuwa mpenzi wa malkia wa runingani, Betty Kyallo amejitokeza waziwazi kuzungumzia tetesi za penzi lao kuvunjika.
Kupitia Instagram, Jones alichapisha
jumbe zenye aya ndefu akionekana kukanusha vikali uvumi wa kuachana kwake na
Betty Kyallo.
Hata hivyo, katika utetezi wake kwamba
penzi lao bado lingali hai, kijana huyo alionekana kulaumu pombe kwa kauli za
awali, akiweka wazi kwamba hatua yake itakayofuata ni kumuomba Kyallo samahani.
Licha ya kutofunga harusi katika ndoa
rasmi, kijana huyo alimrejelea Betty Kyallo kama mke wake akisema kwamba
anamjua kama mtu muelewa ambaye atamsamehe.
“Hakuna mtu ameachwa, hiyo ilikuwa
ni pombe inazungumza. Ninampenda sana mke wangu na sasa naenda kumuomba
msamaha. Kutoka kwa vitendo vyangu, mimi ndiye ninastahili kuachwa na sio
vinginevyo,” Jones alisema.
“Tulijenga haya mahusiano na nyinyi
wajinga mnadhani kwamba huu ndio wakati ambapo mnampa mke wangu ushauri. Wanawake
wenye majungu wanampigia simu wakimuambie eti ‘mrembo unstahili mazuri’,”
Jones alimaliza huku akitamka neno la nguoni.
Uvumi wa kuachana kwao ulifichuka mapema
Alhamisi baada ya wadadisi wa mitandaoni kubaini kwamba wawili hao walikuwa
wamesitisha urafiki wao kupitia kurasa za Instagram.
Kwa zaidi ya mwaka mmoja wamekuwa
wakionyesha mapenzi yao hadharani, na kuamua kuacha kufuatiliana kwenye
mitandao ya kijamii.
Awali, walikuwa wakifuatana kwenye
akaunti zao kubwa za Instagram na mara kwa mara walichapisha picha na video
wakiwa pamoja. Hata hivyo, hatua yao ya hivi karibuni imeacha wengi wakijiuliza
iwapo uhusiano wao uko shakani.
Kijana huyo mwenyewe ndiye aliyeanzisha
uvumi huo kwa msururu wa jumbe kwenye Instagram ambazo sasa ameonekana kujutia.
"Ndio,
tumeachana. Hata akiniaibisha, sitadanganya kuhusu jina lake. Aseme
anavyotaka," aliandika.
Akaongeza: "Usiseme
uongo kunihusu, nami sitasema ukweli kukuhusu."
Charlie pia alipakia meme
ikionyesha kuwa anajitambua kwamba yeye sio mzuri kabisa na hajali jinsi
anavyochukuliwa na watu.
Katika chapisho lingine,
alizungumzia afya ya akili ya wanaume, akieleza kuwa mara nyingi haizingatiwi
hadi mambo yanapozidi kuwa mabaya.
"Hakuna
anayejali afya ya akili ya mwanaume hadi hasira itokee, ndipo kila mtu anaanza
kumwona kama mtu mbaya,"
ilisomeka meme hiyo.
Hata hivyo, katika muda wote huu, Betty
Kyallo amesalia kimya asiweze kuzungumzia suala hilo.