
FAUSTINE Lipuku Lukale, mpiga picha ambaye aliibuka kuwa rafiki wa kipekee aliyesimama na familia ya TikToker Brian Chira wakati wa kifo chake amefunguka yale aliyojifunza wakati na baada ya kifo hicho.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lukale ambaye wengi
wanamfahamu kama Baba Talisha aliungana na mamia ya mashabiki wengine wa
marehemu Brian Chira kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kufa kwake
katika ajali.
Alisema kwamba tangu kifo cha rafiki huyo, amejifunza mambo
mawili makuu, yote yakionekana kurejelea mishale aliyotupiwa baada ya kusimama
na familia yake katika mazishi.
Baba Talisha ambaye aliburuzana na nyanyake Brian Chira siku
chache tu baada ya kuongoza TikTokers wenzake kuchangisha zaidi ya shilingi
milioni 8 kwa ajili ya mazishi ya Chira, alisema kwamba hajutii hata kidogo
fadhila alizoonyesha.
“Mwaka umepita na Leo
inanikumbusha mambo 2 tangu Huyu Kijana Chira aondoke.
1. Usijutie fadhili ulizoonyesha
mtu ambaye hakustahili. Walikukosea, ukawatendea mema, na kwa ajili hiyo
unapaswa kujivuna.
2. Siku moja, mtu
uliyejitolea sana kwa ajili yake atageuka na kusema hakuwahi kuomba, na itaumiza
kwa sababu watakuwa sahihi,” Baba Talisha alisema.
Brian Chira aliaga dunia Machi 16 mwaka uliopita katika kile
kilichoripotiwa na polisi kama ajali ya kugongwa na gari barabarani.
Jumamosi, TikToker mwenzake ambaye mpaka sasa amesalia kuwa
msaada wa pekee kwa nyanyake Brian Chira, Obidan Dela alitembelea familia hiyo
na kurekodi video wakiadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha mpenzwa wao.
Katika video hiyo, Obidan Dela na Watoto hao walikuwa
wameishikilia picha kubwa ya Brian Chira huku wakikumbuka na kukariri kauli
aliyopenda kuitamka ‘kama wewe si pesa huwezi nipa stress’.
Pia waliimba kwa
huzuni wimbo wa Otile Brown ‘One Call’ ambao ulisheheni sana wakati wa mazishi
ya Chira ambapo ilisemekana ulikuwa moja ya nyimbo alizozipenda pakubwa.
“Yo guys, Obidan
Dela hapa, guys, na niko na Brian Chira na Sophie Njeri Chira Kadogo na
wananiambia kama vile Chira alikuwa anawaambia, ‘Kama wewe si pesa, huwezi
ni-stress.’”