Kando ya Hifadhi Maarufu ya Kitaifa ya Maasai Mara nchini Kenya kumesimama kituo cha uokoaji cha Namunyak, hifadhi ndogo lakini yenye uhai kwa wasichana ambao hatima zao hapo awali zilikuwa mashakani. Jina lake, Namunyak, kwa lugha ya Kimaasai linamaanisha "furaha".
Wasichana wanacheza mpira katika Kituo cha Uokoaji cha Namunyak, mji wa Aitong, Kaunti ya Narok, kusini magharibi mwa Kenya, Agosti 31, 2025. (Xinhua/Yang Guang)
Karibu kila wikendi, Tang Lin na Yuan Lin husafiri katika nyika za Maasai Mara wakiwa na gari lililojazwa vifaa – viatu vya michezo, nguo, pipi na mahitaji ya kila siku – kwa ajili ya wasichana 29 walioko chini ya uangalizi wao.
Tang na Yuan, wote wakitokea Chongqing, kusini magharibi mwa China, walikuja Kenya kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kazi katika sekta ya utalii. Kadri idadi ya wageni wa Kichina nchini ilivyoongezeka, biashara yao ikakua. Mnamo 2019, walinunua hifadhi ya ikolojia (eco-lodge) Maasai Mara. Walichokianza kama mradi wa kibiashara kikawa jukumu lisilotarajiwa la huruma.
Wasichana wanacheza mchezo wa chess katika Kituo cha Uokoaji cha Namunyak, mji wa Aitong, Kaunti ya Narok, kusini magharibi mwa Kenya, Agosti 31, 2025. (Xinhua/Yang Guang)
Muda mfupi baada ya kufungua hifadhi yao, mwanamke wa hapa aitwaye Mary Silantoi aliwakaribia.
Akiwa anajitolea katika idara ya kaunti ya masuala ya wanawake na watoto, Silantoi alikuwa amewahifadhi wasichana kadhaa waliotoroka ndoa za mapema au ukeketaji. Aliwaomba nafasi ya kufungua duka dogo katika hifadhi ili kusaidia katika malezi ya wasichana hao.
Kwa mujibu wa ripoti ya serikali ya kaunti, wasichana wenye umri wa kati ya miaka 10 na 19 wanahesabiwa kuwa takriban asilimia 30 ya wajawazito katika eneo hilo. Wengi wao, wakiwa bado watoto, huozwa kwa ng’ombe wachache.
"Nina binti yangu mwenyewe," alisema Tang mwenye umri wa miaka 48. "Nilipoona watoto wakikimbia peku na nikajua kwamba wengi wako nje ya shule, sikuweza kufumbia macho."
"Wenyeji walitusaidia kuanzisha biashara yetu, na tulitaka kurudisha shukrani," aliongeza Yuan.
Wasichana wanatumia simu janja iliyotolewa na watalii wa Kichina kupiga picha za kujipiga (selfies) katika Kituo cha Uokoaji cha Namunyak, mji wa Aitong, Kaunti ya Narok, kusini magharibi mwa Kenya, Agosti 31, 2025. (Xinhua/Yang Guang)
Wawili hao waliamua si tu kusaidia duka la Silantoi bali pia kusaidia kuanzisha makazi ya kudumu na salama kwa wasichana. Uamuzi huo ulisababisha kuanzishwa kwa Namunyak – shirika la kijamii lililojitolea kuwalinda wasichana walio hatarini.
Mnamo Juni 2023, Tang na Yuan walinunua ekari 15 (takriban hekta 6) karibu na mji wa Aitong, Kaunti ya Narok, na kujenga kituo cha uokoaji cha Namunyak. Ingawa ni cha kawaida, kituo hicho kiliwapa Silantoi na wasichana sehemu ya kweli ya kuita nyumbani.
Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, Tang na Yuan wamekarabati makazi ya wasichana, kusakinisha umeme na mnara wa maji, kulipia karo zao, na kuajiri walinzi na walezi.
Karibu na kituo hicho sasa kuna madarasa mapya, jikoni na vyoo, pamoja na vibanda vitatu vya kitamaduni vya nyasi vinavyotumika kama ofisi na makazi ya Silantoi.
Miongoni mwa wasichana hao ni Mitchell Ketere mwenye umri wa miaka 13, aliyejiunga na Namunyak miaka miwili iliyopita baada ya kifo cha baba yake kuacha familia yake ikihangaika. "Nataka siku moja kuwa mpishi. Ninapenda kupikia wengine," alisema kwa tabasamu ang’avu.
Tang Lin (wa 3 kushoto) na Yuan Lin (wa 3 kulia), wadhamini wa Kituo cha Uokoaji cha Namunyak, wakiwa pamoja na mkurugenzi wa kituo hicho Mary Silantoi (katikati), wapiga picha ya pamoja na wasichana katika kituo hicho cha uokoaji, mji wa Aitong, Kaunti ya Narok, kusini magharibi mwa Kenya, Agosti 31, 2025. (Xinhua/Yang Guang)
"Wasichana hawa wamepitia nyakati ngumu, lakini sasa wanang’aa kwa fahari, shauku na matumaini," alisema Silantoi mwenye umri wa miaka 56, ambaye amejitolea kuwafundisha maadili, uthabiti na kujiheshimu. Anaota siku ambayo hakuna msichana atakayehitaji kuokolewa, na kila msichana wa Kimaasai ataishi utotoni salama na yenye furaha.
Mnamo Machi 2024, serikali ya kaunti ilisajili rasmi Namunyak kama shirika la kijamii, ikitambua mchango wake katika ustawi wa eneo hilo.
Kwa Tang na Yuan, safari yao Kenya ni zaidi ya hisani. "Tumetengeneza biashara hapa, lakini pia tumetengeneza familia," alisema Tang. Yuan akaongeza: "Furaha inamaanisha kila binti – awe Kenya au China – anaweza kuishi maisha bora."
Katika nyika pana za Maasai Mara, ambako wanyamapori hutangatanga kwa uhuru, wanaume wawili kutoka China wamepanda mbegu za matumaini. Kwa wasichana 29 wa Namunyak, furaha si neno tena – sasa ni nyumban