

MUIGIZAJI wa muda mrefu wa filamu za Bongo, Wema Sepetu amefichua kwamba yeye anamzidi mpenzi wake, mwanamuziki Whozu kwa miaka 6.
Akizungumza na waandishi wa habari za burudani wakati wa kusherehekea
siku ya kuzaliwa ya Whozu, Wema alikanusha tetesi kwamba anamzidi Whozu jumla
ya miaka 15.
Hata hivyo, alisema kwamba haoni tatizo kuwa katika uhusiano
wa mapenzi na mwanamume ambaye ni mdogo kiumri, akitetea pengo la miaka 6 baina
yao.
Kwa mujiu wa Sepetu, pengo la miaka 6 baina yake na Whozu si
vibaya sana kwani kuna baadhi ya wapenzi ambao wana pengo la hadi miaka 20 kati
yao na mapenzi yanataradadi vyema tu.
Muigizaji huyo alifichua kwamba wamekaa katika uhusiano wa
kimapenzi na Whozu kwa miaka 4 sasa ila akawarai mashabiki wao wanaotamani
kushuhudia harusi yao kusubiri kwa kitambo kidogo.
“Mimi Whozu namzidi kwa
miaka 6 na wala si 15. Nimemzidi miaka 6 ambayo kwangu mimi naona sio mibaya
sana hata kama ingekuwa 10 kwani shida iko wapi? Kuna watu wengine huko
wamezidiana kwa miaka 20-25, sembuse mimi miaka 6 tu!” Sepetu alisema kwa
kujishaua.
“Tuna miaka 4 sasa ya
hivi katika uhusiano, labda niseme hivi kwamba mimi ndoa sio kitu ambacho
nakiota wala kukitamani sana, kwa sababu pia nimeona imeniharibu kisaikolojia
watu wangu wa karibu, ndugu zangu, rafiki zangu nimewaona ndoa zikiwaharibikia.”
“Kwa hiyo sijui nimekuwa
ni muoga lakini mimi nahisi ndoa ni mipango ya Mungu, kama Mungu kawaandikieni
ndoa itakuwa tu, si kitu cha kulazimisha. Cha kushukuru Mungu ni kwamba kuna
upendo ndani mwetu na siku hizi wanasema kwamba mkishaishi pamoja miezi 3
tayari ni kama mmeoana,” Wema Sepetu alisisitiza.
Wema alitetea uhusiano wake na Whozu akisema kuwa mtu yeyote
hata kutoka kwa familia yake ambaye ana shida na uhusiano wake na Whozu basi
nilo ni kwao wala si kwake.
Alirejelea tukio la miaka miwili iliyopita ambapo mamake
alifoka vikali kukata uhusiano wa bintiye na Whozu ambaye alimuona kama kijana
ambaye hajakomaa kuwa katika penzi na mwanawe.





