
CHARLIE Jones, kijana Gen Z ambaye ni mpenzi wa mwanahabari wa runinga ya TV 47, Betty Kyallo ameibuka kwa mara nyingine na dai la kujinyenyekeza kwa mama huyo wa binti mmoja.
Jones bila kuona aibu alipeleka kwenye instgram yake kueleza
jinsi penzi lake na Betty Kyallo limekolea munyu kiasi kwamba kuachana ni ndoto
ya alinacha.
Alifichua kwamba kila siku anaporauka asubuhi, jambo la
kwamba analojikumbusha na kushukuru ni kwamba ni mmoja kati ya vijana wachache
wenye wanawake warembo.
Pia alidai kwamba yeye yuko radhi kutii kila amri ya Betty
Kyallo, akijitaja kama mbwa mtiifu ambaye atabweka mpaka kukuche ikiwa mmiliki
wake (Kyallo) ataamrisha hivyo.
Pia alisema kwamba yuko tayari leo-kesho kufasnya chochote
ambacho Kyallo atamtaka kufanya, ikiwa ni pamoja na kufanya shughuli za ndani
hadi kuchota maji.
"Ni asubuhi nyingine
nijikumbushe kuwa nilipata mke motomoto. Mimi ni mbwa wake Akisema enda chota
ninachota Anasema kubweka? Nitabweka woof woof woof hadi mtaa mzima
uamke," Charlie alieleza.
Haya yanajiri siku chache baada ya Charlie kuyeyusha mioyo na
ujumbe wa siku ya kuzaliwa kwa Betty alipofikisha miaka 36 Jumamosi, Machi 15,
2025.
Katika heshima yake, alimtaja kama moyo wake, amani yake, na
baraka zake kuu.
"Sijui hata nianzie
wapi kwa sababu maneno hayatawahi kutosha kuelezea jinsi ninavyokupenda. Wewe
ni moyo wangu, amani yangu, baraka yangu kubwa. Wewe ndiye mtu wa kuchekesha
zaidi ninayemjua- ndio, mcheshi zaidi kuliko mimi (nitakubali mara moja tu).
Jinsi unavyochukia sana, kunifanya nicheke hata wakati sitaki, ni jambo la
kushangaza kuhusu wewe. Kama, unaonekanaje mzuri hata kwenye pyjamas, sio sawa,” alisema.
Ujumbe huu ulikuja siku chache baada ya kijana huyo mdogo
kuzua wasiwasi kwamba penzi lake na Kyallo liliporomoka.
Hata hivyo, katika kujieleza, alisema kwamba ujumbe huo
ulishawishiwa na ulevi, akisisitiza kwamba yeye na Kyallo hawawezi kuachana
kiboya.
Aliwageuzia mtutu wa mashambulizi wale ambao walionekana
kusherehekea penzi lake na Kyallo kusambaratika, akisema kwamba aibu inasalia
kwenye panda la nyuso zao.